HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 08, 2021

WAZIRI MKUU AWASHUKURU WATANZANIA

 


 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania kwa kuwa watulivi na kudumisha Amani na mshikamano katika siku 21 za Maombolezo ya Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati  Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 Mwaka huu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salamu.

Akiongea na waandishi wa habari leo  Jijini hapa Amesema ikiwa leo tarehe 7 ya mwezi wa 4 ndio siku ya Mwisho ya Maombolezo  na kupeperusha bendera nusu mlingoti Watanzania waliokuwa wametulia wakiuzunika na nchi ikiwa kwenye kilio kikubwa.

Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa miongozo na taratibu juu ya Maombolezo  kwa muda wa siku 21 na bendera kushushwa nusu mlingoti.

"Baada ya matangazo na miongozo iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zoezi ya kuandaa  Mipango ya mazishi yalianza ikiwemo kuaga mwili wa hayati Magufuli Jijini Dar es Salamu, Dodoma, Zanzibar,Mwanza, Chato na mpaka siku anasikwa," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Na kuongeza kuwa " Leo napenda kushukuru makundi mabalimbali bila kusahau serikali ya Zanzibar kwa ushiriki wao  kwa kuhakikisha maandalizi  hadi siku ya kumzika  Hayati Dkt Magufuli," amesema.

Akishukuru Makundi Mbalimbali.

Akitoa Salamu zake za Shukrani kwa Makundi Mbalimbali amewashukuru wakuu wa Mikoa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama,Jeshi la Akiba ,Skauti na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Halmashauri na Kamati Kuu ya CCM ,Uviccm kwani hayati Magufuli ndio alikuwa Mwenyekiti wao kwa kufanya kazi kubwa .

Shukrani kwa Familia.

Amesema Wanashukuru wanafamilia wa Hayati Magufuli akiwemo Mjane Mama Janeth Magufuli ,Watoto ndugu jamaa na marafiki wa karibu kwa utulivu walioonyesha kipindi chote cha Msiba.

Vyombo vya Habari.

Amemshukuru Vyombo vya Habari kwa kutoa na kuhabarisha kwani wameweza kusaidia wananchi kufuatilia vipindi chote vya Msiba kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali.

Hata hivyo amewataka hofu wananchi kwa kusema miradi yote ya Maendeleo iliyopangwa kutekelezwa utaelekezwa  taarifa zitaendelea kutolewa kwa kila hatua.

No comments:

Post a Comment

Pages