NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
MAWAZIRI wa Nchi za Afrika zinazozalisha Madini ya Almasi wamekutana Jijini Dodoma na kufanya mkutano wao wa 7 ambapo mkutano huo utaendeshwa na kuhitimishwa kwa njia ya video .
Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Waziri wa Madini Dotto Biteko wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema lengo la mkutano huo wa siku mbili ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.
Mkutano huo wa siku mbili utahusisha ushiriki wa Mawaziri na waataalam wa Madini kutoka nchi 12.
"Tanzania ndiye nchi mwenyeji wa Mkutano huo na kwamba itapokea Uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Namibia ambayo inamaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja," amesema.
Pia amezitaja nchi zinazoshiriki Mkutano huo kuwa ni pamoja na Angola,Afrika ya kusini,Namibia ,Tanzania,Zimbabwe,Togo,
Aidha Katika Mkutano huu ,pia kuna nchi saba ambao ni waangalizi ,nchi hizo ni Aljeria,Jamhuri ya Congo,Code D’lvore,Gabon,Liberia,Mali na Maurititania.
Pia amesema kuwa,kupitia mkutano huo watapata fursa ya kubadilishana uzoefu nan chi wanachama wengine kuhusu usimamizi wa Sekta ya Madini na kuimarisha utendaji katika Wizara ya Madini.
“Katika kipindi cha uenyekiti wetu tutajitahidi kuhakikisha kuwa tunaboresha mifumo ya Jumuiya ya hii ili iweze kuwa na manufaa kwa nchi wanachama kama inavyokusudiwa,”amesema.
kuhusu malengo ya Jumuiya hiyo amesema ni pamoja na kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zoteza Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama.
“Sasa kupitia jukwaa hili nchi zinapata fursa ya kubadilishana taarifa za uzoefu katika sekta ya madini na kujenga uwezo wa wataalamu kuhusiana na masuala ya Almasi ," Amesema.
No comments:
Post a Comment