Meneja
Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (wa pili kulia) akiwaelekeza maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa kwenye simu janja alipofanya nao kikao cha maandalizi ya kwenda kutoa mafunzo ya kuijengea uwezo jamii ya wafugaji katika Kitongoji cha Mogelo wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Mifugo, Abbas Mubanga, Afisa Kilimo, Issa Mwambela na Afisa Ushirika, Grace Samwel.
Na Mwandishi Wetu
JAMII ya
wafugaji ambao wengi wao ni wamasai kupatiwa mafunzo na Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara wa Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ya
kuwajengea uwezo kiuchumi jinsi ya kuboresha mifugo yao na kilimo kwa
kutumia hati miliki za kimila kama dhamana kukopea fedha benki na
taasisi zingine za kifedha.
Akizungumza
wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo hayo, kilichohudhuriwa na
maafisa wa Halmashauri ya Wilaya Mbarali, mkoani Mbeya, Meneja
Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema mafunzo
hayo yanafanyika katika Kitongoji cha jamii ya wafugaji cha Mogelo kesho
Mei 27,2021.
Ametaja
mafunzo watakayopatiwa kuwa ni; kuboresha mifugo yao, Kanuni za kilimo
bora, kuthaminisha mali zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu za mahesabu,
faida za ushirika, kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa
kutumia hati miliki za kimila kama dhamana, faida za kujiunga na mabenki
kwa ajili ya mikopo na ufugaji bora wa nyuki wa asali.
Kabla
ya kikao na maofisa hao, Temu alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha
na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii
hiyo ya wafugaji.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment