Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuanzisha umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Mzumbe (ALUMNI), Prof.
Ganka Nyamsogoro, akiongoza kikao kilichojumuisha wanafunzi waliosoma chuo hicho kilichofanyika jijini Zanzibar.
Kikao cha Kamati Maalum ya kuanzisha umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Mzumbe (ALUMNI), kikiendelea jijini Zanzibar.
UNGUJA, ZANZIBAR
Chuo kikuuu cha Mzumbe (Mzumbe University) kimekusudia kuanzisha umoja wa wahitimu waliosoma katika chuo hicho (Alumni Association).
Hayo aliyasema Prof. Ganka Nyamsogoro ambaye ni mwenyekiti wa kamati maalum ya kuanzisha umoja huo wakati akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa Zanzibar waliosoma katika chuo hicho huko katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) katika Campus ya skuli ya Kompyuta na Mafunzo ya Habari kilichopo kilimani katika mkutano wa kupokea maoni ya kuazisha katiba pamoja na sera za Jumuiya hiyo.
Alisema umoja huo utaundwa na wahitimu wote waliotokana chuo hicho tangu jina la Institute of Development Management ikiwa maarufu IDM Mzumbe hadi Mzumbe University wenye lengo la kuhakikisha wahitimu wanashiriki katika shuhuli za maendeleo katika Chuo hicho.
Alisema umoja huo unaojulikana kwa jina la Alumni Asociation wahitimu watafaidika na umoja huo kwa kuwa sehemu moja ya chuo hicho.
‘’Tukifanikiwa kuusimamisha umoja huu na kuendeleza wahitimu wataweza kupata mafunzo ya muda mrefu kwa vitendo katika maeneo tofauti ‘’alieleza
Sambamba na hayo alisema wahitimu hao watakapokuwa katika umoja huo wanaweza kushirikiana na chuo ili kuleta maendeleo.
Profesa alieleza kuwa kupitia umoja huo chuo kitatambuwa kazi ambayo imefanywa na muhitimu aliyotoka katika chuo hicho na kuitangaza.
‘’Lengo letu ni kuona licha ya wahitimu kupata elimu lakini pia watatangazwa kutokana na kazi zao wanazozifanya’’alieleza.
Alisema chuo kinakusudia kupitia umoja huo kuthamini kazi kupitia wahitimu wake popote walipo duniani ikiwa ni mfanya biashara au mwana michezo kuzitangaza kazi zao.
Alisema kupitia umoja wao huo wanaweza kutoa mchango wa maendeleo kwa kutolea mfano wa kujenga mabweni kama ni sehemu ya kulipa fadhila waliyopata katika chuo hicho.
Chuo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kikijulikana kwa jina la IDM hadi kufikia 2001 kilichopewa jina la MZUMBE UNIVERSITY ambacho tayari kina wahitimu zaidi ya elfu ishirini.
Chuo hicho ambacho Mkuu wake ni Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa wahitimu wa chuo hicho.
No comments:
Post a Comment