HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2021

MAKAMU WA RAIS AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI NANYUMBU

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 24, 2021 amefanya ziara ya kustukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliopo Wilaya ya Nanyumbu.

 

Makamu wa Rais amekasirishwa na uongozi wa Wilaya kufanya upotevu mkubwa wa fedha  usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo.


Makamu wa Rais amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika.

 

Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.

 


Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya mara baada ya kukagua majengo ya stendi ya mabasi ya Mangaka. Makamu wa Rais aliagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi kufuatia matumizi mabaya ya fedha za mradi huo. (Picha na VPO).

No comments:

Post a Comment

Pages