HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 17, 2021

Meya kumbilamoto azindua TaWoE, awahimiza wanawake wa sekta ya nishati kufanya kazi kwa bidii

 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TaWoE).

  

Mwenyekiti wa Mtandao wa taasisi hiyo Mhandisi Gwaliwa Mashaka, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TaWoE) pamoja  na programu zilizomo katika mtandao huo.

 

Picha ya pamoja.

 

Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto amewahimiza wanawake wanaofanya shughuli zao katika sekta ya nishati nchini kutokata tamaa badala yake wajenge utamaduni wa kujiamini ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo na kukuza uchumi wa nchi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TaWoE) pamoja  na programu zilizomo katika mtandao huo.

Akizindua mtandao huo amesema wanawake wote wanaojishughulisha na shughuli za nishati wana umuhimu mkubwa katika kuchochea maendeleo ya nchi hivyo wana jukumu la kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa bidii ili kuchangia uchumi wa nchi.

Amebainisha kuwa kwa kutambua mchango wa sekta hiyo tayari tayari jiji limeshatenga asilimia nne ya mapato inayokusanya kuwasaidia wanawake na kwamba ataiunga mkono taasisi hiyo lengo likiwa kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea.

" Mchango wa sekta binafsi unafahamika naomba nichukue fursa hii kuwapongeza wanawake wote wanaounda TaWoE msikate tamaa fanyeni kazi zenu kwa weledi na bidii muikuze sekta na uchumi wetu," amesema Meya Kumbilamoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa taasisi hiyo Mhandisi Gwaliwa Mashaka  amesema mwitikio wa wanawake katika seta hiyo ni mzuri huku akibainisha hadi sasa wana wanachama 200.

Mhandisi Gwaliwa amesema bado kuna changamoto zinazowakabili wanawake waliopo katika sekta hiyo ikiwemo kutoaminiwa kwa kutopatiwa tenda na kusisitiza kuzinduliwa mtandao huo kutawasaidia kujitangaza na kupata masoko ya bidhaa za nishati

Naye Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Nishati na Madini ambaye pia ni Mshauri Muelekezaji masuala ya umeme wa kampuni  ya Gein Energy  Product  Farm Dkt.Juliana Pallangyo amesema sekta hiyo ina wanawake wengi wanaofanya kazi zao kwa bidii hivyo ameiomba Serikali kuziamini kampuni za nishati za wanawake kwa kuzipatia tenda za miradi.


No comments:

Post a Comment

Pages