Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani (CCM), Hawa Mchafu (kushoto )
akikabidhi matofali kwa uongozi wa Chama kwa ajili ya ujenzi wa
ofisi ya CCM Kata ya Magindu. (Picha na Victor Masangu).
NA VICTOR MASANGU, MAGINDU
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu katika kuhakikisha
anatekeleza ilani ya Chama ameamua kuchangia matofali Mia 500 kwa ajili
ya ujenzivwa ofisi ya CCM kata ya kibindu iliyopo halmashauri ya
kibaha vijiji.
Mchafu
amekabidhi matofali hayo kwa uongozi wa Chama ngazi ya kata kwa ajili ya
kuanza ujenzi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa viongozi wa CCM
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Katika
ziara hiyo Mchafu aliongozana na viongozi mbali mbali wa Chama ngazi ya
Wilaya pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya UWT katika halmashauri
ya kibaha vijiji kwa lengo ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
Pia
alisema ameamua kufanya ziara yake ya kikazi kwa kutembelea katika
maeneo mbali mbali ikiwemo mkuranga.kibiti.kibaha mji pamoja na kibaha
vijijini pamoja na kutoa msaada wa mifumo ya saruji pamoja ya michanga
ili kusaidia sekta ya elimu,afya,pamoja na kusaidia wanawake
wajasiriamali na vikundi.
Pia
alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kwamba
inawasaidia wananchi kuweza kuwapa sapoti ya kuwawezesha kiuchumi ili
waweze kuondokana na wimbi la umasikini.
Akiwa
katika ziara yake katika halmashauri ya kibaha vijijini pia aliweza
kupata fursa ya kutembelea kikundi cha kufyatua matofali kilichopo kata
ya mtongani na kutoa msaada wa mifumo 25 ya sarufi.
"Ndugu
zangu nipo katika ziara yangu ya kikazi katika mkoa wa Pwani na lengo
langu kubwa ni kupita katika baadhi ya Wilaya kugagua miradi ya
maendeleo sambamba na kuchangia mifuko ya saruji katika kusaidia
maendeleo katika nyanja tofauti;"alisema Mchafu.
Kadhalika
aliwaomba wanachama wa Chama Cha mapinduzi hususan wanawake wa UWT
kuendeleza ushirikiano naye kwa nia ya kuleta mapinduzi katika suala
zima la maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani.
Katika
hatua nyingine alikutana na viongozi mbali mbali wa CCM kata ya magindu
ili kusikilizwa kero na changamoto zinazowakumba ili kuzitafutia
ufumbuzi.
Baadhi ya
viongozi wa CCM kata hiyo ya magindu walimueleza Mbunge huyo kuwa Kuna
changamoto katika baadhi ya maeneo ikiwemo suala la ukosefu wa maji Safi
na salama pamoja na ukosefu wa madaktari katika zahanati yao ya
kibindu.
Akijibu hoja
hizo Mbunge Mchafu aliwaahidi wananchi hao na viongozi changamoto hizo
amezichukua na kwamba atahakikisha anazifanyia kazi na kuzifikisha
katika mamlaka zinazo husika.
Kwa
upande wao badhi ya viongozi. CCC katika halmashauri ya kibaha vijijini
walimpongeza kwa dhati Mbunge huyo kwa kuwachsngia mifuko ya saruji
katika kujenga ofisi ya kata ya kibindu na kukisaidia kikundi Cha
kufyatua matofali.
Awali
Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Michael Mwakamo alisema anamshukutu
Mchafu kwa kuamua kufanya ziara yake iliyoambatana na neema ya utoaji wa
mifuko ya saruji ambayo italeta tija katika kukuza maendeleo.
No comments:
Post a Comment