HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2021

TMDA: Uhamasishaji wa kutoa taarifa madhara ya dawa umeleta mafanikio

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Dawa  na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo amesema katika uhamasishaji wa kutoa taarifa madhara yatokanayo na dawa kwa jamii  mwitikio umekuwa mkubwa ikilinganishwa na kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam mkurugenzi huyo amesema  kipindi cha miaka mitatu iliyopita walikuwa wakipokea ripoti 100 hadi 200  ya madhara yatokanayo na  dawa kwa mwaka.

Fimbo amesema ripoti hiyo ilikuwa inawapa shida kutokana na idadi ya watu waliopo Tanzania kwani walihitaji angalau ripoti 10,000  hadi 12,000 kwa mwaka.

" Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO),linataka angalau tupokee ripoti 1000 katika 100,000, kwa hiyo kuanzia miaka mitatu iliyopita tulikuwa tunapokea ripoti kati ya 8000 ambayo ni mafanikio makubwa ya mamlaka kupata ripoti hii kwa mwaka,"ameongeza.

Tunaamini ni kwa sababu ya juhudi ambazo tulizifanya kuhamasisha jamii, wataalamu wa afya, Wafamasia, madaktari manesi na  wanaotoa taarifa mara kwa mara," ameeleza Fimbo.

Amebainisha kuwa wamekuwa wakifanya uhamasishaji kwa kipindi cha muda mrefu kupitia watu binafisi, wagonjwa na wale wanaojihusisha na huduma za afya kwa ajili ya kutoa taarifa ya madhara ya dawa.

Mkurugenzi huyo amesema mwitikio wa kutoa taarifa ni mkubwa kutokana na mbinu mbalimbali walizotumia mfano
 Teknolojia ya Habari, Mawasiliano (TEHAMA),simu za kiganjani na kupitia tovuti ya mamlaka hiyo.

" Mwitikio wa matumizi ya kielekroniki kwa Tanzania mafano simu za kiganjani imechangia na kuchagiza kwa kiasi kikubwa utoaji taarifa madhara ya dawa, " amesema Fimbo

Amesema wameona imeongeza idadi waliyohitaji kuwa kubwa kwa sababu kisayansi kunatakiwa  kuwa na ushahidi wa kutosha kusema dawa fulani ina madhara.

" Ukikosa taarifa iliyokuwa ya kimaaandishi  huwezi kusema dawa ina madhara. Kazi yetu kubwa ni kudhibiti kama imefikia hatua ya kusababisha madhara kwa watu wengi  lazima dawa iondolewe  kwenye soko isitumike kwa kuwa inadhuru," ameongeza.

Au kuweka lebo kwenye dawa mfano dawa hii isitumike kwa watoto ama kwa watu wenye tatizo la figo, moyo au wenye historia mbalimbali ya maradhi  yanayowasumbua," amesema Fimbo.

Fimbo amesema lengo la kuweka lebo ni kumkumbusha mtumiaji kwamba endapo ana maradhi hayo haruhusiwi kutumia dawa hiyo.

" Kazi yetu Kwanza tunawasiliana moja kwa bmoja  na watumaji dawa tunawaelekeza kwa mfano dawa hii ikitumika Tanzania imekuwa ikileta nadhara haya, hivyo badilisheni lebo huko huko kiwandani zikiletwa ziwe zinaletwa zile ambazo zinatoa masharti ya matumizi," ameongeza.

Nyinyi kama waandishi wa habari pia mtusaidie kuelimisha jamii vizuri ili tutumie wataalamu wetu kwa sababu mambo ni ya kitaaluma yanahitaji lugha ya kitaalamu,' amesema.

Amesema dawa zinawasaidia watu na kazi yake ni kutibu magonjwa mbalimbali hivyo lazima zitumike na kwamba zikileta madhara ambayo hayakubaliki TMDA huchukua hatua ya kuzizuia.

No comments:

Post a Comment

Pages