Mmoja wa wazazi aliyefika katika banda la Chuo Kikuu cha Zanzibar akipata maelezo na fursa zinazopatikana katika chuo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Zanzibar Idara ya Biashara- Kitengo
cha Uhasibu na Fedha, Dkt. Salama Yusuf.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chuo
Kikuu cha Zanzibar (ZU) kimewakaribisha na kuwashauri wazazi wenye
watoto waliomaliza Kidato cha nne, sita, ngazi za cheti, astashahada na
shahada kuhudhuria katika banda lao la Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi
na Teknolojia ili wapatiwe elimu ya orodha ya kozi zinazofundishwa na
walimu na wataalamu wa idara waliobobea.
Hayo
yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo hicho katika Idara ya Biashara- Kitengo
cha Uhasibu na Fedha, Dkt. Salama Yusuf kwenye maonesho hayo
yanayoendelea Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema
wazazi watakaofika katika banda lao watapata fursa ya kupewa elimu ya
kozi zinazowafaa kusoma watoto wao kulingana na ufaulu walionao kutoka
kwa walimu na wataalamu wa idara waliopo hapo na kwamba chuo hicho kina
mazingira bora ya kujisomea.
" Wazazi
wahudhurie hapa bandani watapatiwa elimu sahihi ya kozi tutoazo
zinazowafaa watoto wao tuna walimu na wataalamu waliobobea tuna
mazingira bora ya kujisomea watapohitimu watatoka wakiwa mahiri katika
taaluma walizosomea," amesema Dkt. Salama.
Amebainsha
kuwa katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu
chuo hicho kimeanzisha kozi ya ujasiriamali katika ngazi ya cheti na
shahada kuwasaidia wahitimu kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.
Amesisitiza
kuwa chuo kinazingatia kanuni na miongozo ya wizara ya afya kwani
katika maeneo ya chuo hicho kilichopo Tunguu nje ya Mji wa Zanzibar
wanafunzi, walimu na wakuu wa idara wanavaa Barakoa, upakaji vitakasa
mikono, ukaaji wa mita moja madarasani pamoja na meneo mengine.
Ameipongeza
TCU kwa kuendelea kuandaa maonesho hayo kwani yanatoa fursa adhimu kwa
vyuo vikuu na taasisi kujitangaza na utoaji elimu kwa wanafunzi
wanaofanya udahili wa masomo wa mwaka 2021/22 huku akiishauri tume hiyo
kuboresha mfumo wa mtandao wake ili ufanye kazi kwa haraka.
Dkt.
Salama amezitaja kozi mbalimbali zinazofundishwa na chuo hicho katika
ngazi mbalimbali ikiwemo Usimamizi wa Biashara, Maendeleo ya Jamii,
Sheria, Biashara ya Teknolojia, Ustawi wa Jamii, Uuguzi na Ukunga,
Ushauri wa Saikolojia, Masoko, Uhasibu, Sayansi katika Uuguzi,Utawala
pamoja na Sanaa katika Uchumi.
No comments:
Post a Comment