Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali Vicky Bishubo, akiaangalia Meza na viti kabla ya kumkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Suleiman Jaffo kwa ajili ya Shule ya
Sekondari Mzenga, Kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki,
Harold Lambileki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazimngira, Suleiman Jaffo, akipongezwa na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari
Mzenga baada ya kupokea Meza na viti vilivyotolewa na Benki ya NMB wakati wa
hafla iliyofanyika Kisarawe jana. Katika ni Mkuu wakitengo cha Biashara za Serikali Vicky
Bishubo Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la
Kisarawe, Justina Kikuli. Benki ya NMB kupitia mpango wake wa
uwajibikaji kwa jamii ( CSR) ilikabidhi madawati na mabati kwa shule ya ya Msingi Chanzige A na ya Sekondari Mzenga zote zikiwa wilayani kisarawe.
Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB ,Vicky Bishubo,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Sulemani
Jafo, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki, Harold
Lambileki, Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Chanzige A pamoja na wanafunzi wakiwa wameshika moja ya bati zilizokabidhiwa kwa shule ya Msingi Chanzige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoa Pwani.
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Seleman Jafo,
ameitaja Benki ya NMB kuwa ni Taasisi inayoitendea haki Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na watu wake kupitia Program ya Uwajibikaji kwa
Jamii (CSR) na ukubwa wa gawio la benki hiyo kwa Serikali linalotokana
na hisa zake.
Waziri Jafo
ameyasema hayo Ijumaa ya Julai 30, wakati akipokea msaada wa viti 50,
meza 50 na mabati 165, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 10,
vilivyotolewa na NMB kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mzenga na Shule ya
Msingi Chanzige A, zilizoko wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Kauli
ya Waziri Jafo, inakuja huku NMB ikiwa imetumia zaidi ya Sh. Bilioni
1.1, kusaidia utatuzi changamoto mbalimbali kwenye Sekta za Elimu na
Afya kuanzia Januari hadi Julai 2021, kati ya Sh. Bil. 2 ambazo ni
asilimia 1 ya faida yake ya mwaka uliopita, ambazo zinatumika kutoa
misaada mwaka huu, ambao pia imekabidhi serikalini gawio la Sh. Bilioni
21.76.
Akizungumza katika
hafla hiyo iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige A, mjini
Kisarawe, Waziri Jafo alisema ukubwa wa kiasi cha Sh. Bil. 2 ilizotenga
NMB kusaidia nyanja za Elimu na Afya, unathibitisha namna benki hiyo
inavyoiishi kaulimbiu yao ya Karibu Yako.
"Kiasi
hicho kinaenda kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu
Hassan kutatua kero mbalimbali katika elimu na afya, nyanja ambazo
zinanufaika pia na Mipango ya Maendeleo ya Serikali kupitia bajeti zake,
zinazopewa nguvu pia na ukubwa wa gawio la NMB kutokana na hisa zetu
kwao.
"Kwa dhati, niseme
NMB mnaitendea haki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake, kwani
hamjawahi kuwa nyuma katika kuisapoti Serikali kutatua kero za jamii,
hii inawafanya Watanzania kujivunia uwepo wenu. Tuliziomba taasisi
nyingi, Ila nyie mkawa wa kwanza kutujibu na leo kutukabidhi misaada
hii," alisema.
Waziri
Jafo, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, aliipongeza NMB kwa kazi kubwa
inayofanya kila uchao wilayani humo, huku akiiomba kuendelee kusaidia,
sambamba na kuangalia uwezekano wa kujenga tawi dogo la benki hiyo huko
Maneromango, ili kuwaondolea wananchi na watumishi wa umma adha ya
kutembea na pesa kufuata huduma za kibenki mjini Kisarawe.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitenho cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky
Bishubo, alimhakikishia Waziri Jafo kuwa changamoto za Sekta ya Elimu na
Afya ni kipaumbele cha benki yake, kutokana na ukweli kuwa elimu na
afya ndio ufunguo, msingi na mtaji mkuu wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja
na Taifa kwa ujumla.
"NMB
tunatambua juhudi za Serikali kusimamia elimu na afya kwa nguvu zote
kwa kuboresha mazingira ya utoaji huduma hizo mijini na vijijini, na
tunaipongeza. Pamoja na jitihada hizo, sisi kama wadau, tunajiona tunao
wajibu wa kuunga mkono kuikwamua jamii, ambayo inatufanya NMB kuwa benki
kubwa na bora kuliko zote nchini," alisema Bishubo katika hafla hiyo.
Naye
Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Harold Lambileki, aliishukuru
Serikali wilayani Kisarawe kwa ushirikiano inaouonesha kwa benki yake na
kuahidi kuudumisha kwa maendeleo endelevu ya Kisarawe, huku Katibu
Tawala wa Wilaya hiyo, Mwanana Msumi, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya,
akisema inatambua na kuthamini mchango wa NMB kwa ustawi wa wilaya na
wananchi wake.
No comments:
Post a Comment