HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

October 21, 2021

DC Mwaipaya ashiriki maonesho ya Kilimohai

MKUU wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Abdallah Mwaipaya akisaini kitabu cha wageni cha Mkulima Mbunifu kwenye banda la Shamba la Kilimo Oganiki lililopo kwenye kijiji cha Kwanyange wilayani Mwanga.

Na Irene Mark

Banda hilo ni moja ya mabanda mengi yaliyoshiriki maonesho ya bidhaa za kilimo hai na kongamano la siku mbili la kimataifa la kilimo ikolojia na kilimo oganiki lililoanza leo Oktoba 20.2021 jijini Dodoma.

Mwaipaya amefurahishwa na shughuli zinazofanyika kwenye shamba hilo na kupokea maelezo ya namna jarida la Mkulima Mbunifu linavyowasaidia wakulima huku akiahidi kuchukua nakala za jarida hilo na kuwapelekea wakulima wa wilayani kwake.

No comments:

Post a Comment

Pages