Na Mwandishi Wetu
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amewapongeza Wachezaji wa zamani wa
ligi mbalimbali za soka kwa kuandaa Bonaza la mchezo huo
lililofanyika Jana jijini Dar es Salaam.
Mwegelo alikuwa Mgeni
rasmi wa Bonanza hilo lililofanyika viwanja vya Gwambina Lounge zamani
TTC Chang'ombe na kushuhudia mbungu la wakongwe likimwagika vya kutosha.
Alisema
michezo ni Afya na ni jambo jema kuona wachezaji wa zamani amabao
walisakata kabumbu kwa nyakati zao wanaendelea na michezo jambo ambalo
linaendelea kuwafanya wawe na afya njema.
"Kwanza kabisa
niwapongeze waandaaji wa Bonanza hilo mmefanya jambo kubwa sana lakuweza
kukusanyana na kuweza kukumbushia enzi za ubora wenu naamini hili ni
jambo kubwa linalopaswa kuungwa mkono.
Pia alionyeshwa
kufueahishwa kuweza kuwashuhudia wakongwe ambao walikuwa na mastaa enzi
za uchezaji wao na kuweza kulitumikia taifa kwa uaminifu mkubwa."
Bonanza
hilo lilikusanya wachezaji wa zamani hufanyika Kila mwaka mwezi oktoba
14 siku ya kaudhimisha kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Wachezaji hao wa zamanj ni muunganika wa wachezaji wa madaraja tofauti ambao wamepata kucheza.
Lengo
la kuanzishwa kwao umoja wa wachezaji wa zamani The Galaticos ni kuweza
kuwa pamoja katika kusaidiana katika shida na Raha Ili kuenzi undugu na
Urafiki pamoja na kuenzi utumishi wao katika Soka.
Vilevile ni kuweza kukutana na kuzungumza Juu ya muelekeo wa Soka la Nchi kwa kutoa ushauri pale unapohitajika.
Nae
Mwenyekiti wa wachezaji wa zamani Ally Mayay alisema umoja huo umekuwa
nguzo ya kutatua changamoto za wachezaji wa zamani na kuwaweka pamoja .
"Bonanza
la wachezaji wa zamani ambalo limetufanya wachezaji wastaafu kucheza
soka kwenye madaraja tofauti, siku za mwanzo tulikuwa wachezaji wa ligi
Kuu tu lakini baadae tukasema hata wachezaji walio cheza daraja la
kwanza hata kama la tatu ilimradi tu ligi iliyokuwa inatambulika"
alisema na kuongeza kuwa
"Hili tumelifanya baada ya kuona
wachezaji wengi wanaishi kinyonge baada ya kustaafu, kwaiyo
tukatengeneza kitu ambacho wenyewe tutakuwa tunajitegemea, na kiukweli
toka tumeanzisha umoja huu kuna misiba mingi sana ambayo watu
wamesaidiana, kwa mfano mchezaji akifiwa na Baba, Mke sijui Mtoto
anapewa Milioni moja, lakini anapswa kuwa mwanachama hai ambaye analipa
Ada, analipa michango ya misiba lakini pia wanasaidia Ada za wachezaji
ambao wanataka kusomea ukocha, mechi kamishina kwaiyo umoja huu
unasaidia sana"
"Umoja huu umewafanya wachezaji kuwa pamoja
walikuwa wanaalikwa tu kwenye mabonanza, likubwa ukaribu na kuanzia
mwenyekiti mpaka mjumbe Wote ni Wachezaji wa zamani, kwaiyo haujachukua
mtu ambaye ni nje ya wao wenyewe. Kama watakosea kujiongoza ni wao
wenyewe. Alisema Ally Mayay Mwenyekiti wa Wachezaji wa zamani The
Galaticos.
No comments:
Post a Comment