Wadau wa Bima.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kamishna
wa Bima Nchini Dkt. Mussa Juma amewataka Mawakala wa Bima Nchini
kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima
ili kufikia malengo ambayo Serikali imejiwekea ikiwemo kufikia asilimia
80% ya uelewa wa bima kwa wananchi,huku akibainisha angalau asilimia
50 ya Watanzania wawe wamepata Bima mojawapo kufikia mwaka 2030.
Kamishna
Mussa ametoa wito huo jijjini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo ya
siku mbili yaliyoandaliwa na Umoja wa Chama Cha Mawakala wa Bima Nchini
ambayo yamelenga kutoa elimu juu ya namma Bora ya kuendesha
uwakala,kutafuta masoko pamoja na kufahamu mambo ya kodi kuhusu Bima
hatua ambayo itawasaidia wakala hao kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Kamishna
huyo wa Bima kutoka ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini ( TIRA)
amesema kwamba ili kufikia malengo hayo ni muhimu mawakala,madalali
pamoja na makampuni ya Bima kuendelea kutoa elimu kwa wateja, kuuza
bidhaa za Bima kulingana na uwezo wa kampuni zao pamoja na kushughulikia
na kutatua haraka migogoro ya Bima inayojitokeza kwa wateja wao.
"Kujiendeleza
kielimu inasaidia kuwa nauelewa mpana katika masuala ya Bima hususani
mambo ya teknolojia na hii inawasaidia msiachwe nyuma kwenye
ushindani,hivyo jitahidini Kila mmoja awe na kitu cha kipekee ili
unaeshindana nae asiweze kukushinda ,kwahiyo mnapata semina hii
kuwafanya msitupwe kwenye ushindani"amesema.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Chama Cha wakala wa Bima Nchini Sayi Daudi ameiomba
serikali kuondoa sharti la kuwekea kiwango cha fedha benki (FDR) ambacho
kitatumiwa na wakala kulipa gharama za bima pindi atakapokutana na
changamoto za kutenda nje ya utaratibu kwa mteja wake nakwamba sharti
hilo limekuwa kikwazo Kwa wakala wa bima ambao ni wapya.
" Tunaiomba serikali iondoe hiki kigezo kinachomtaka mtu anaetaka kutoa huduma za bima lazima awe na kiasi fulani cha fedha
benki ambacho kinaweza kutumika kumlipa mteja anaetendewa kinyume cha
utaratibu, jambo hili limekua kikwazo kikubwa Kwa wakala wa
bima,tunaiomba ikiwezekana waiondoe " amesema Sayi ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya FIDES Insurance iliyopo Dar es salaam.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi watendaji wa makampuni ya wakala wa Bima
akiwemo Bi.Modesta Liviga wa Kampuni ya Primode Insurance Agency.
pamoja na Bw.Meshack Matulile Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BMC Insurance
Agency wamesema kwa nyakati tofauti kuwa mafunzo hayo yatawasaidia
kufahamu namna bora ya kuuza bidhaa za bima, kutafuta Masoko ya Bima
hatua ambayo itasaidia kufanya kazi zao Kwa ufanisi mkubwa.
No comments:
Post a Comment