Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisisitiza jambo kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula amezindua Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania
(Tanzania International Cycle Tour) jijini Dar es Salaam.
Mashindano
haya ambayo yatafanyika sambamba na Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa
Tanzania yanalenga kutambua mchango wa Tanzania katika kupigania
Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika na kusherekea mafanikio
yaliyofikiwa na Tanzania katika demokrasia, amani na utulivu wakisiasa
tokea kupata Uhuru kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa katika barani Afrika.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo Waziri
Mulamula ameeleza imani yake kuwa kupitia mashindano hayo yakipekee
ujumbe wa Mshikamano na Umoja ambao unabeba dhana nzima ya Maadhimisho
ya miaka 60 ya Uhuru utawafikia watu wengi zaidi.
Aidha
ametumia nafasi hiyo kutoa Wito kwa Taasisi zingine kutoka Nchi
Wanachama wa Afrika Mashariki kuiga jambo lililofanywa na waandaaji wa
Shindano hili ambao ni Taasisi ya Afrika Mashariki Fest na Taasisi ya
Utalii wa Utamaduni Butiama.
“Tunaamini
pia baada ya mashindano haya mtakuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa
kuwa mkiwa huko njiani wakati wa mashindano mnaenda kujionea mabaliko
makubwa ya maendeleo kijamii na kiuchumi na mafanikio makubwa
yaliyofikiwa na Nchi yetu katika nyanja mbalimbali” alieleza Waziri
Mulamula.
Nae
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema amefarijika sana namna vijana
kutoka nchini, Jumuiya Afrika Mashariki na nchi nyingine nje ya Jumuiya
walivyohamasika kushiriki katika Mashindano haya. Aliendelea kueleza
hiki ni kielelezo tosha kuwa vijana wanatambua na kudhamini uhuru wao
sambamba na kudhamini jitihada zinazofanywa na Serikali yao katika
kuleta maendeleo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utalii wa Utamaduni
Butiama Bw. Godfrey Madaraka Nyerere ameeleza kuwa pamoja na mambo
mengine mashindano haya yanaenda kuionesha dunia hatua kubwa ya
maendeleo iliyofikiwa nchini katika ujenzi wa miundiumbinu ya uchukuzi
hivyo kuleta mchango mkubwa katika kutangaza Utalii sambamba na kuvutia
Uwekezaji kutoka Nje.
Katika
hafla hiyo ya ufunguzi wa Mashindano pamoja na washiriki wengine
ilihudhuriwa na Mhe. Tabia Maulid Mwita Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mabalozi na
Wanadiplomasia kutoka Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki
wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini, Bw. Kisembo Ronex Tendo Mtendaji
Mkuu wa Afrika Mashariki Fest kutoka nchini Uganda na Bw. Godfrey
Madaraka Nyerere Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utalii wa
Utamaduni Butiama
No comments:
Post a Comment