HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2021

Mikoa 14 kupata mvua kidogo kwa miezi sita


Dk. Kijazi akitangaza utabiri wa msimu Dar es Salaam leo Oktoba 27,2021.

 

 Na Irene Mark



MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi amesema mvua za msimu unaoanza Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022 zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Akizungumza na wanahabari leo Oktoba 27,2021 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Kijazi amesema mikoa itakayopata mvua hizo haba ni ile yenye msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

“Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa maeneo mengi ya mikoa hii itapata mvua za chini ya wastani.

“Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

“Utabiri unaonesha kuwepo kwa vipindi virefu vya ukavu vinavyotarajiwa kati ya Novemba,2021 na Januari,2022 hata hivyo ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa mwezi Machi 2022,” amesema Dk. Kijazi.

Amesema mvua hizo za msimu zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya Novemba, 2021 katika maeneo mengi na kuisha kati ya wiki ya pili na ya tatu ya Aprili, 2022.

Dk. Kijazi alitoa tahadhari na ushauri wa kuwepo kwa upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo unaitarajiwa kuwepo katika maeneo mengi yanayopata mvua za msimuvna kuathiri ukuaji wa mazao.

Pia ametahadharisha kupungua kwa kina cha maji katika mito, mabwawa na hifadhi ya maji ardhini kinatarajiwa kupungua hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za chini ya wastani.

Amesema mlipuko wa magojwa unatarajiwa kujitokeza kutokana na upungufu wa upatikanaji wa maji safi na salama.

 Amezishauri mamlaka kuchukua tahadhari na kuwaeeza wananchi hatua za kuchukua kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment

Pages