HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 21, 2021

MLIPA KODI ASIYEZINGATIA MATUMIZI YA MASHINEZA KIELEKTRONIKI (EFD) KUTOZWA MILIONI 3 IKIWA NI PAMOJA NA KIFUNGO JUU YAKE

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata akitoa ufafanuzi juu ya wajibu walionao  wafanyabiashara.

 


 Na Lydia Lugakila, Bukoba

.
Wafanyabiashara biashara Mkoani Kagera wametakiwa kuwa na matumizi sahihi ya ya mashine za kielektroniki -EFD ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi yake huku walipa kodi wasiozingatia kukumbana na sheria za kodi kwa kwani adhabu yake ni shilingi milioni 3 kwa kila kitendo kimoja na kifungo juu yake au vyote kwa pamoja.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Alphayo Kidata katika mkutano na wafanyabiashara wakubwa na wa Kati Mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mkoa huo.

Kidata amesema kuwa wakati wafanyabiashara hao wanakumbushwa kulipa kodi kwa hiari wanatakiwa kuzingatia mambo makuu muhimu ikiwa ni pamoja kuzingatia utunzaji wa kumbukumbu za biashara zao, kwani inasaidia katika ukadiliaji na ukusanyaji wa kodi,  hivyo ni muhimu kwani kunawawezesha maafisa wa TRA kukadilia kodi stahiki na serikali kupata kodi kwa stahiki bila dhuruma.

" Wafanyabiashara mnatakiwa kuwa na matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki (EFD) mshine hizi zina uwezo wa kuandika majina na namba ya utambulisho wa mnunuzi wa bidhaa hivyo wasiotumia mashine hizo wamo hatarini" alisema Kamishna huyo.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia ulipaji wa kodi ya serikali  kwa hiari bila kutumia matumizi ya nguvu, huku wakitengeneza mipango ya kulipa madeni ya nyuma ikiwa ni pamoja na kujiepusha na biashara ya magendo kwani muhusika anapokamatwa Mali zake utaifishwa pamoja na vyombo vinavyotumika kusafirishia bidhaa hizo hivyo kuwahimiza kutumia mipaka rasmi ili kuondokana na kufirisiwa hadi kifungo kwa wahusika.

Amesema kuwa mashine za EFD zinapoharibika mfanyabiashara anatakiwa kutoa taarifa ili kubadilishiwa  mashine nyingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema ulipaji wa kodi ya serikali ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani sheria ya Mamlaka ya kodi Tanzania sura ya 3 namba 399 iliyoanzishwa na TRA inaeleza majukumu ya Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kukadilia na  kukusanya mapato ya serikali.

Meja Jenerali Charles Mbuge amewapongeza walipa kodi Mkoani humo kwa kuendelea kutekeleza sheria ya kulipa kodi kwa hiari na kuwaomba kuendelea na uzalendo huo ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya Tehama katika kutoa huduma ya ukusanyaji wa kodi kwa mifumo hiyo inarahisisha ulipaji wa kodi kwa hiari.

Kufuatia hali hiyo amemuhakikishia Kamishna wa Mamlaka hiyo kuwa uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na ofisi yake itaendelea kusimamia maendeleo ya serikali juu ya ukusanyaji wa kodi huku akitoa pongezi kwa TRA Mkoani Kagera kwa namna wanavyojidhatiti katika kukusanya kodi, na kuwahimiza kuzingatia haki za walipa kodi na wakusanya kodi kuzingatia wajibu wao ikiwemo kila mfanyabiashara kutumia mashine za EFD kwa usahihi.

Hata hivyo kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara Mkoani Kagera Radislaus Jerad amekemea suala la magendo  na kukiri kuwa linafanyika kwa kificho jambo linalowaathili wafanyabiashara na kuikosesha serikali kupata mapato.

No comments:

Post a Comment

Pages