HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 20, 2021

WAHITIMU UDSM WATAKIWA KUTUMIA ELIMU WALIYOIPATA KUJIAJIRI


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Rais Mstaafu Dkt. Mrisho Kikwete.

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
 
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa Mahafali ya 51 wameaswa kutumia elimu waliyoipata kujiajiri, kuwa chachu mabadiliko katika jamii, kutatua matatizo ya jamii, wazalendo, kudumisha hadhi ya chuo pamoja na kuwa wepesi kutafuta fursa zitazowasaidia kujikwamua kimaisha.

Aidha, Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais Mstaafu Dkt. Mrisho Kikwete ameupongeza uongozi wa UDSM kwa kupiga hatua katika usawa wa jinsi kwa wahitimu wa shahada za awali waliohitimu chuoni kwa mwaka wa masomo 2020/21.

Awali akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Anangisye amewaasa wahitimu kutumia elimu yao kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa na Serikali pamoja na kuzitafuta fursa zilipo.

" Tumieni elimu yenu kuwa chachu ya mabadilko ya jamii msisubiri kuajiriwa  muwe tayari hata kufanya kazi za kujitolea muende mkatunze hadhi ya chuo hiki, amesema Pofesa Anangisye.

Amebainisha kuwa chuo hicho kimepata mafanikio makumbwa ikiwemo kupata kiasi cha Billioni 3 kwa ajili ya kufanya utafiti na ubunifu,pamoja nakuanza kudahili wanafunzi kutoka mataifa yakigeni kwa ajili ya kujifunza lugha ya Kiswahili.

Kwa upande wake Mwayekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) Jaji Mstaafu Damian Lubuva ameshukuru hatua zinazochukuliwa na Rais  Samia kujikinga na uginjwa wa Uviko 19, nakutumia fursa hiyo  kusema kuwa chuo kinaendelea kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

"Nyinyi wahitimu na wale mnaobakia nawaomba muendelee kuchukua tahadhali kama tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa uviko 19, rais amekuwa mstari wa mbele kutukumbusha haya na sisi tuendelee kumuunga mkono" amesema Jaji Mstaafu Lubuva.


 

No comments:

Post a Comment

Pages