HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 25, 2021

TAKUKURU BUKOBA YAANZA KUMCHUNGUZA AFISA UVUVI


 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge  akiwa na viongozi mbali mbali wa Mkoa huo pamoja na wavuvi waliotelekezwa.

 

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kagera imeanza uchunguzi dhidi ya afisa uvuvi mfawidhi anayedaiwa kuhusika na tukio la kuwatelekeza wavuvi 9 na  kupotea ndani ya Ziwa Victoria kuanzia Oktoba 9 mwaka huu.

Watu hao 9 wanadaiwa kupotea ndani ya ziwa Victoria manispaa ya Bukoba  wakiwa hai ambapo baada ya kuwasili muda mfupi kutokea nchi jirani ya Uganda wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera mnamo oktoba 9 mwaka huu wavuvi hao wakiwa na wavuvi wengine wanadiwa kukamatwa na Afisa uvuvi mfawidhi kutoka kikosi cha doria cha mkoa huo Yohana kwa madai kutofuata sheria za uvuvi ambapo inadaiwa aliyachukua kwa nguvu matenki ya mafuta ya kuendeshea mitumbwi yao na kisha kuondoka huku akiwatelekeza ziwani bila msaada wowote.

Mbuge amesema kuwa alipokea taarifa za kupotea kwa wavuvi hao mnamo Oktoba 12 mwaka huu na kumwita katika ofisi za mko huo mahojiano ambapo afisa huyo amekana kuhusika na tukio hilo.

" Nilimuita huyo Bwana ofisini kwangu nikamhoji akasema yeye hahusiki na tukio hilo" alisema Meja Jenerali Charles Mbuge.

Aidha kufuatia tukio hilo Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani humo imekwisha anza uchunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo  mkuu huyo wa Mkoa amewaonya watendaji wa serikali wenye tabia ya kuwaonea na kuwanyanyasa  wananchi kuacha tabia hiyo mara moja badala yake wafuate sheria pale wanapowakamata na makosa wavuvi hao.

No comments:

Post a Comment

Pages