HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 25, 2021

WFP yawasaidia wakulima kuuza mtama Sudani Kusini


 Neema Sitta Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP), akizungunza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu baadhi ya shughuli za WFP hapa Tanzania.

 

Na Irene Mark, Dodoma


WFP yawasaidia wakulima kuuza mtama Sudani Kusini

MPANGO wa Chakula Duniani (WFP), umefanikiwa kuwaunganisha wakulima wa mtama zaidi ya 22,000 na soko la uhakika la zao hilo nchini Sudani Kusini.


Wakulima hao wanafanya kilimo hai cha mtama wanatoka kwenye wilaya sita kati ya saba za Mkoa wa Dodoma ambapo kati ya  Januari,2021 hadi Septemba,2021 walikuma hao wameuza tani 17,000 za mtama na kupata zaidi ya Sh. Bilioni tisa. 


Akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wakati wa kongamano la pili la kimataifa la Kilimo Ikolojia na Kilimo Hai, Mkuu wa Ofisi Ndogo ya WFP, Neema Sitta alisema ofisi yake inawawezesha kulima na kuwapa masoko ya uhakika wa mazao hayo.


“Kwa mwaka huu pekee tumeuza tani 17,000 kutoka wilaya tatu kati ya sita tunazofanya nao kilimo cha mtama. Wilaya hizo ni Bahi, Mpwapwa na Kongwa.


“WFP kwa kushirikiana na Serikali tumeamua kuuheshimisha mtama na kuwainua wakulima. Miaka miwili nyuma kilo moja ya mtama iliuzwa sh. 250 sasa hivi mkulima anauza kilo moja kwa Sh. 550.


“Tukefanikiwa kuondoa madalali waliokuwa wanamnyonya mkulima, WFP tunamsaidia mnunuzi kufika shambani, mkulima anaona thamani ya kazi yake anaishika pesa ambayo hakutegemea,” anasema Sitta.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa ofisi ndogo, wakulima wapo chini ya Program ya miaka mitano iitwayo Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA) inayotekelezwa WFP kuanzia mwaka 2017 hadi Juni, 2022.


Sitta anabainisha kwamba CSA imewafikia wakulima 22,000 kwenye vijiji 203 kati ya vijiji vyote 700 vya wilaya sita zinazofanya mradi huo wa WFP.


Akifafanua shughuli zinazofanywa na WFP, Sitta alisema ni mpango unaofanya kazi kwa mtazamo wa kibinadamu hasa kwa kuisaidia serikali kwenye  sekta za kilimo, maendeleo, wakimbizi, afya na lishe ambapo kwa Dodoma wamewekeza kwenye kilimohai cha mtama kwa kuongeza usalishaji na masoko.


“Uwekezaji huu kwenye kilimohai au kilimo himilivu uliongezewa nguvu na Shirika la Maendeleo la Ireland (Irish Aid), lililowekeza Sh bilioni 1.7 kwenye mradi wa CSA.


Alisema mkulima hupewa elimu sahihi ya matumizi ya ardhi na namna ya kutengeneza mbolea na viuadudu kwa njia za asili katika kufanya kilimohai.


Wilaya nyingine zilizopo kwenye mradi wa CSA wa WFP ni Chemba, Kondoa, Dodoma na Chamwino.

No comments:

Post a Comment

Pages