HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2021

TAMIDA champongeza RC Makalla, SGL chawasisitiza wadau wa madini kujiunga uanachama


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini Tanzania (TAMIDA) ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji wa GEM TANZANITE LTD, 
Osman Tharia, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini Tanzania (TAMIDA) kimempongeza Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam RC Amos Makalla kwa kutembelea Ofisi ya Soko la Madini la mkoa huo, kuzindua ofisi ya chama hicho pamoja na kuahidi kutoa ushirikiano utakaochangia kuboresha soko hilo kulifanya liwe na hadhi Kimataifa.

Aidha, chama hicho kimeishukuru na kuipongeza Kampuni ya Wanunuzi Wakubwa wa Dhahabu Nchini ya SAB GOLD LIMITED (SGL) kwa kufadhili ofisi ya TAMIDA huku kikisistiza kampuni hiyo imekuja kuwakomboa wadau wa sekta ya madini wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo, wachimbaji wa madini hasahasa dhahabu pamoja na madalali.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GEM TANZANITE (GT), Osman Tharia amesema kuwa wadau wa sekta hiyo kupitia TAMIDA chini ya ufadhili wa kampuni hiyo watatafutiwa masoko ya bidhaa zao, kuunganishwa na wafanyabishara wengine, utoaji ushauri na elimu ya namna ya kuchimba, kuandaa na uuzaji wake.

" Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza RC Makalla kutembelea soko la madini na kushiriki kuzindua ofisi ya TAMIDA  ametuahidi kutupa ushirikiano wenye malengo ya kuliboresha soko liwe la kimataifa na tija kwa Tanzania," amesema Tharia.

Amebainisha kuwa chama hicho kupitia SGL kimejipanga kuwafikia wadau wa madini nchi nzima lengo likiwa kuwakomboa kwa kuzifanya biashara zao zifahamike nchini na katika masoko ya kimataifa.

Amewasisitiza wachimbaji wadogo, wafanyabiashara kujiunga uanachama wa chama hicho ili waweze kufaidika nacho kwani wasipojiunga mambo yanayohitajika kufanyiwa hayatatimia.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imekuja na mwelekeo imara ambao utawakomboa wadau wa dhahabu huku akifafanua SGL itanunua bidhaa zao kwa bei yenye manufaa katika masoko. 

No comments:

Post a Comment

Pages