Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku wakuu wa mikoa na wakurugenzi kusafiri nje ya mikoa yao bila kibali kutoka kwa Rais,Makamu wa Rais au Waziri Mkuu lengo nikusimamia kwa ukaribu matumizi ya mkopo wa Trilioni 1.3 uliotolewa na shirika la Fedha Duniani (IMF )kwaajili ya mapambano dhidi ya Uviko 19 na utekelezaji miradi ya maendeleo.
Ummy ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati akitoa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo za IMF kwa upande wa mamlaka ya serikali za mitaa wamepatiwa jumla ya shilingi Bilioni 535.6 ambazo zimegawanywa katika maeneo matatu ikiwa ni pamoja na Elimu, Afya na Kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Ummy ameelekeza fedha zinazokwenda kwenye elimu wakurugenzi na wakuu wa shule kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa madarasa na vifaa vyake bikamilike kabla ya tarehe 15.12.2021.
Kwa upande wa Afya amesema wanakwenda kusimika mitambo ya kisasa ya utoaji huduma za kibingwa.
Na kwa eneo la kuwawezesha wananchi kiuchumi fesha hizo ziende kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya wafanyabiashara.
Aidha amelekeza viongozi wote wa mikoa kuhakikisha wanaweka alama katika majengo yote yatakayojengwa kwa mkopo huo wa IMF ili kuonyesha utekelezaji wake kwa vitendo kwakua viongozi watakaoshindwa kufanya hivyo watapelekwa moja kwa moja TAKUKURU.
No comments:
Post a Comment