Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Jim Yonazi amewapa maagizo matatu watoa huduma za posta ikiwemo kuleta ubunifu nini cha kufanya ili kuboresha huduma za posta nchini
Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya posta pamoja na kupeleka mapendekezo ya kile ambacho kimefanyika katika sekta hiyo.
Akizungumza leo, Jijini Dodoma wakati akifungua warsha ya watoa huduma za Posta,Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mkutano huo ni muhimu hivyo amewapa maagizo ya kuleta ubunifu nini cha kufanya ili kuboresha huduma za posta nchini.
Pia ameyataja Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya posta pamoja na kupeleka mapendekezo ya kile ambacho kimefanyika katika sekta hiyo.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabir Bakari amesema warsha hiyo ni muhimu kwani watoa huduma hao wamekuwa wakitoa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka eneo moja mpaka jingine.
Maadhimisho ya wiki ya Posta Duniani yameanza rasmi Jana na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 9 Mwaka huu.
October 09, 2021
Home
Unlabelled
WATOA HUDUMA ZA POSTA WATAKIWA KUWA WABUNIFU
WATOA HUDUMA ZA POSTA WATAKIWA KUWA WABUNIFU
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment