HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 08, 2021

NHIF: Tupo tayari kuwahudumia Watanzania wote


 Meneja Mahusiano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Angela Mziray.
 

NA BETTY KANGONGA

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema upo tayari kuwahudumia watanzania mara baada ya Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utakapopitishwa bungeni.

Hivi karibuni Serikali ilisema kuwa itaanza kutekeleza Mpango wa Bima ya Afya kwa wote kwa kutenga Sh.Bilioni 149 katika mwaka wa Fedha 2021/22

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Angela Mziray kwenye Maonesho ya Wiki ya huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali imeamua kuwahudumia Watanzania waweze kupata huduma za afya bora kwa kujenga vituo vya afya na kuboresha huduma hizo na ndio maana imekuja na Mpango huo.

Mziray alisema, Serikali imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya ili kuboresha miundombunu ya kutoa huduma ya afya hivyo ni vema watanzania wakaendelea kujiunga na bima ya afya kwa kuwa gharama zimepunguzwa na zipo katika makundi mbalimbali.

Amesema NHIF imejiandaa kuhakikisha inaweka mfumo wa Tehama ambapo watanzania wataweza kujisajili popote walipo kutokana na urahisi utakaokuwa umewekwa.

Kuhusu maonesho hayo Meneja Uhusuano huyo amesema katika kipindi cha siku saba katika maonesho hayo watatoa huduma mbalimbali ikiwemo ya usajili kwa watu wanaotaka kujiunga na Mfuko huo.

Aidha amesema watatumia muda huo kutoa elimu wa wakazi wa Jiji la Dar es salaam kujua umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya badala ya kusubiri kuugua ndipo wakate.

No comments:

Post a Comment

Pages