HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2021

YALIYOJIRI JIJINI DODOMA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hatua mbalimbali ilizochukua wizara hiyo kuwafikishai barabara na usafiri wa majini  sehemu zao tangu kupatikana kwa uhuru hadi leo.

Waziri MkuuKassim Majaliwa, akisoma hotuba yake ya kulifunga bunge jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Mbongwe CCM, Nicodemus Maganga, akisoma majina ya wapiga kura wake Bungeni baada ya kuomba mwongozo kwa Spika kwa wananchi wake wanaodaiwa kuuawa na wavamizi wa maeneo yenye madini akidai wanasaidiwa na baadhi ya maofisa wa Serikali.
 Mbunge wa Mbongwe CCM, Nicodemus Maganga, akitulizwa na wabaunge wenzake baada ya kushindwa kuendelea kutoa maelezo yake na kuanza kulia.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba ndani ya ukumbi wa bunge kabla ya kuliahilisha bunge leo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, akizungumza na wabunge ndani ya ukumbni wa Msekwa jijini Dodoma, Wizara hiyo iliwaandalia warsha wabumnge kuwafahamisha mambo mbalimbali ya wizara hiyo.

 

Maofisa wa Wizara hiyo  na wabunge wakisikiza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na katika warsha hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara CCM, Regina Ndege, akiuliza swali katika kipindi cha maswali na majibu bungeni leo.


Wandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa, Makame Mbarawa, alipokuwa akitoa maelezo ya wizara yake miaka 60 ya Tanzania Bara tangu kujitawala.


Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, akiuliza swali katika kipinci cha maswali na majibu cha bunge leo.


Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi (kushoto), akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais IKULU Kapteni Mstaafu George Mkuchika, mazungumzo hayo yalifnayika ndani ya ukumbi wa bunge.


Wanakwaya wa Bunge wakisubili kuimba wimbo wa Taifa na Wimbo wa Afrika Mashariki baada ya kuahilishwa bunge na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


No comments:

Post a Comment

Pages