Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dk. Gwajima akiweka shada wakati wa msiba wa kijana Egidi Gangata, aliyefariki dunia kwa kuchomwa na kisu jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
VIONGOZI ngazi ya mkoa na halmashauri, kata, mitaa, kijiji na vitongoji wametakiwa kujipanga upya kutekeleza mwongozo ambao ulizinduliwa wa Mpango Kazi wa Kupambana na Ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Mwongozo huo ulizinduliwa mwaka 2017/2018 ambao umeelekeza kuundwa kwa Kamati za Mapambano kuanzia Kitongoji, Mtaa, Kijiji, Halmashauri, Mkoa na Taifa.
Pia serikali itachukua hatua zote dhidi ya waliohusika na kusababisha kifo cha myoto huyo.
Hayo yalisemwa jijini Dodoma leo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk. Dorothy Gwajima kwenye msiba na mazishi ya Marehemu Egidi Gangata aliyekuwa akishi mitaani aliyefariki kwa kuchomwa kisu maeneo ya Nyerere Square jijini hapa Dk. Gwajima amesema wadau wote waliopo ngazi husika wakijielekeza kupambana na mifumo inayosababisha kujitokeza kwa ukatili ikiwemo inayopelekea watoto kuishi mitaani.
Dk. Gwajima ameeleza kuwa
serikali itachukua hatua zote dhidi ya waliohusika na kusababisha kifo cha myoto huyo.
Mwanga wa Milele Umwangazie Eee Mungu, apumzike kwa Amani Milele, Amina.
Amesema tukio hilo na mengine ya aina hiyo yanadhihirisha haja ya Kamati hizi kuongeza kasi ya kufanya kazi.
"Natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ikiwemo asasi za kiraia, kidini, sekta binafsi, watafiti, wadau wa maendeleo na jamii kuungana na serikali kutafuta suluhu ya kudumu inayoendana na mazingira yetu na rasilimali zetu na ubunifu wetu," amesema.
Amesema Wizara itaratibu mkutano wa kitaifa wa wadau kwa lengo la kupata maoni yao juu ya ufumbuzi wa suala hilo hatimaye wasiwe na watoto wa mitaani badala yake waimarishe mifumo ya makuzi na malezi bora.
Dk. Gwajima amesema wakikubali kuendelea na maisha ya kuwaona watoto wa mitaani ni kujiandalia hatari mbele kama taifa hivyo lazima wapate ufumbuzi wa kudumu.
"Kifo cha marehemu Gangata kitupe mtihani tukatafute majibu mapya na mbinu mpya shirikishi. Baada ya salaam hizi, naomba tumwombe Mungu aipumzishe roho ya Marehemu kwa Amani," ameongeza Dk.Gwajima.
Aidha Waziri huyo ametoa wito kwa jamii nzima ya Tanzania, kifo hivho kiwe funzo na wito wa kutuhamasisha kama jamii kuungana ili kuwafikia wengine ambao wanatamani kuishi maisha mapya lakini wamekosa fursa ambazo zipo ili watimize ndoto zao.
No comments:
Post a Comment