Mwakilishi wa chama chama Cha madalali Tanzania Benson Chamlesile akizungumza na waandishi wa habari.
CHAMA cha Madalali wa Mahakama Tanzania kimewahudumia watu zaidi ya 250 wenye changamoto mbalimbali za kisheria tangu kuanza kwa maonesho ya wiki ya Makahama ambayo inafanyika katika viwanja vya Nyerere square jijini Dodoma.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu "Zama za Mapindizi ya nne ya Viwanda. Safari ya Maboresho Kuelekea Mahakama Mtandao" ambayo yaliaza Januari 23 hadi 29 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma jana katika maonesho hayo Mwakilishi wa chama hicho Benson Chamlesile alisema pia wametoa elimu ya uelewa wa utekelezaji wa amri ya Mahakama.
Chamlesile kuwa wanatekeleza amri ya Mahakama ilivmwenye haki anapata haki yake na kwamba bila wao haki za wanajamii hazitapatikana
Akizungumzia ugumu wa kazi hiyo ya udalali alisema wakati mwingine wanalazimika kutumia nguvu na kwamba wakienda eneo husika wananchi hawana uelewa wa amri za Mahakama.
"Changamoto nyingine ni wakati mwingine shauri kuendeshwa upande mmoja na upande mwingine unakuwa hauna taarifa. Sisi hatushuguliki na mwenendo wa kesi sisi ni utekelezaji tukifika eneo husika tunatekeleza tulichoandikiwa kwenye oda," alisema.
Aliongeza kuwa chama hicho ni mdau wa Mahakama ambao wanatekeleza amri ya mahakama na kusambaza nyaraka katika Mahakama za Tanzania wananzia ya mwanzo hadi kuu
"Chama hiki kimesajiliwa kisheria na tumepata mafunzo yanayoendeshwa na chuo Cha utumishi wa sheria. Tunafanya kazi za utekelezaji wa amri zote za mahakama katika kesi za madai namba 1 na kesi za talaka," alisema.
Kwa upande wake mteja aliyefika katika banda hilo Bodar Awadhi Ahmed alisema kuwa alifika katika banda hilo la chama cha Madalali ambapo alipata msaada wa kisheria ambao unaugusa jamii moja kwa moja.
"Nimepata elimu nzuri kutoka kwa mdogo wangu hapa amenielekeza vizuri maelekezo ya kisheria ambayo yatanisaidia," alisema.
Aliongeza kuw atawashauri wanachi kwenda katika banda hilo ili nao waweze kupata elimu ya masuala ya sheria.
No comments:
Post a Comment