HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA SHERIA

 

RAIS WA  TANZANIA  SAMIA SULUHU HASSAN

UONGOZI wa Mahakama ya Tanzania, umesema Rais  Samia Suluhu Hassan anatarajia kuongoza sherehe za siku ya Sheria Februari 2, badala ya Februari Mosi, 2022 iliyovyopangwa awali.

Hatua ya kuahirisha sherehe hizo ukifanyika Februari Mosi,2022 imetokana na sababu zisizoweza kuzuilika na kwamba zitafanyika katika Viunga vya Chinangali, jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Mahakama, Tiganya Vicente, alisema mhimili huo unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages