Na Asha Mwakyonde, Dodoma
MKURUGENZI wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema atatuma kikosi kazi kuhakikisha mapagale yote ya muda mrefu yanaondolewa lengo likiwa ni kuliweka jiji hilo safi.
Huo ni mwendelezo wa zoezi la ufanyaji wa usafi kwenye Kata na Mitaa yote ya jiji hilo.
Haya aliyasema jana jijini hapa wakati wa zoezi la ufanyaji wa usafi katika Kata ya Kikuyu maeneo ya St. John alisema amesema mapangale na vichochoro vimeonekana vikificha vichaka na uchafu .
"Timu yangu itakuja kutembelea kata hii kutembea tena hapa katika kata hii ili kuangalia ni viwanja gani vina mapagale ya muda mrefu na vilivyosababisha vichaka na uchafu wa muda ,"aliongeza Mafuru.
"Na ni kwanini tunakuwa na mapagale ya muda mrefu katika jiji letu na kwenye Hati kuna sheria inayosema pagale kukaa ni miaka mitatu liwe limejenga jengwa," alisema.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri alisema usafi unaepusha maradhi ni wajibu wakila mwanachi kujitafakari na kujituma katika zoezi la ufanyaji wa usafi katika eneo linalomzunguka.
Pia alifafanua kuwa watakaa siku ya Jumamosi ili kuangalia namna ya kufunga maduka kwa undani zaidi wafanyabiasha wamekuwa wakifunga maduka na kwenye zoezi la usafi hawafanyi.
Naye Diwani wa kata hiyo Israel Mwasansu amesema suala la usafi ni endelevu kuanzia kwenye kaya hadi kwenye jumuiya na kwamba zoezi la usafi ni ustarabu wa mtu hivyo kila mmoja ajitoe kufanya usafi maeneo yanayonzunguka ili kuhakikisha jiji la Dodoma linakuwa safi na la kupendeza.
No comments:
Post a Comment