HABARI MSETO (HEADER)


January 29, 2022

Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa miaka mitano wazinduliwa


 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza kabla ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/ 2026.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/ 2026 wenye lengo la kutoa elimu hiyo kwa makundi yote maalumu.

Akizungumza jijini Dodoma leo  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakati wa uzinduzi Profesa Eliamani Sedoyeka amesema mkakati huo umejumuisha makundi yote maalum kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu.

Katibu huyo amesema mkakati huo ni muhimu na utawapatia dira ya maendeleo kielimu na kwamba utasaidia upatikanaji wa wanafunzi wa awali na wale ambao hawajaanza shule.

Prof. Sedoyeka amesema mpango wa serikali ni kila mtanzania anapate elimu bora bila kujali hali aliyo nayo.

"Elimu Jumuishi kuna makundi 17 na tangu Uhuru mwaka 1961 kama nchi kipaumbele chetu ni kutoa elimu," amesema Prof. Sedoyeka.

Prof.Sedoyeka ameongeza kuwa mkakati huo utawajengea  uwezo watunga sera na kuhamasisha  utoaji wa elimu.

Ameongeza kuwa elimu jumuishi ya awamu iliyopita ilizingatia elimu ya Msingi na elimu ya sekondari na kwamba mkakati Jumuishi wa awamu hii umezingatia katika ngazi zote za elimu.

Hata hivyo,amesema mpango huo ni katika kuhakikisha wanafunzi wanajengewa uwezo na kuimarisha ukusanyaji wa taarifa .

Ametoa wito kwa wadau wote wa elimu Tanzania kuwa wanafikisha taarifa sahihi umuhimu wa elimu Jumuishi ili kila mtu anakuwa na haki ya kupata elimu ikiwemo makundi ya watu wenye mahitaji maalum.

Naye Kamishna wa Elimu Tanzania  Dk.Lyabwene Mtahabwa    amesema kila mtu ana haki ya kupata elimu bora na kumnyima mtu elimu bora ni kumwandaa kuwa mtumwa katika karne hii ya 21.

kupitia Umakini wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuweka kipaumbele upatikanaji wa elimu kwa makundi yote ni vyema kila   mmoja  kuunga jitihada za utoaji elimu bora.

Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu Magreth Matonya amesema katika mkakati huo itakuwa inafanyika tathmini ya mar kwa mara .

Kwa upande wake  katibu wa chama cha Mapindizi (CCM), Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema Wizara hiyo imefanya jambo jema kuanzisha elimu jumuishi kwa watoto wote  kwa kuona nao wanauwezo kupata elimu hiyo kama watoto wengine.

"Kama CCM tutaenda kuhamasisha wazazi wa wenye watoto wa makundi maalumu na mwaka huu tunachaguzi za ndani ya chama hivyo tutahamasishana," amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages