Na Asha Mwakyonde, Dodoma
MKURUNGENZI Msaidizi Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Alexander Mtawa amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa sehemu ya juhudi za mapendekezo ya maboresho ya kanuni za ada na tozo katika kurahisisha ufanyaji biashara hapa nchini wenye lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi na kujenga usalama na mazingira kwa ujumla.
Dkt. Mtawa ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha pili cha wadau kwa ajili ya mapendekezo ya kanuni za ada na tozo amesema kuwa maboresho hayo yemelenga kuboresha sekta ya afya na mazingira ili kuepuka hatari ya mionzi ambayo imeshuhudiwa katika maaeneo mengi Duniani.
"Tunamshukura Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kwa juhudi zinazofanyika ili kuhakikisha nchi yetu inasongambele na wakati huo huo soko la nje la bidhaa Tanzania zinaendelea kulindwa," ameeleza.
Mkurungenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Tanzania(TAEC), Profesa Lazaro Busagala amesema kuwa kikao hicho ni cha pili ambapo cha kwanza waliketi jijini Arusha mwaka jana kwa ajili ya mapitio ya kanani za ada na tozo.
Amesema kuwa kikao hicho kilikubali mapendekezo yote ambayo walipeleka na kwamba kikao cha pili maboresho yamekuwa mazuri zaidi kwa mfabyabiashara kwa sababu kikao kilichopita kile kiwango ambacho kilikuwa kinatozwa kwa asilimia 0.2, kilikuwa kimepunguzwa kikawa asilimia 0.18.
"Kikao cha leo (jana),pendekezo ni kupubguza zaidi,ni kikao ambacho hatutegemei wadau kukataa na wakati huo huo tumependekeza kuwa na viwango ambavyo mfanyabiashara mdogo hatatozwa chocote ila atapata huduma," amesema Prof. Busagala.
Prof.Busagala amesema kuwa anaamini mapendekezo hayo wadau watayatafakari na kwamba mahali ambapo wanatarajia kurekebisha watasikilizwa maoni yao.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau 25 kutoka sekta binafsi,Taasisi za serikali na wawakilishi tokawizara mbalimbali.
Tume hiyo ya Nguvu ya Atomiki ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 7 ya mwaka 2003, awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Mionzi ilivyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 5 ya mwaka 1983 na miongoni mwa majukumu yake ni kudhibiti matunizi salama ya Mionzi nchiniz kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia, kufanya utafiti, kutoa ushauri na kutoa Taarifa mbalimbali juu ya sanyansi na Teknolojia ya Nyuklia.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao cha pili cha maboresho ya ada na tozo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment