Msemaji wa sekta ya Maji na Mazingira ACT Wazalendo, Esther Thomas akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23,2022.
Na Arodia Peter, Dar es Salaam
Chama cha ACT Wazalendo kimemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo kujiuzulu wadhifa wake kutokana na mkanganyiko wa taarifa kuhusu athari za mazingira kwenye Mto Mara mkoani Mara.
Chama hicho pia kimeomba mamlaka za uteuzi kuangalia upya utendaji wa Waziri huyo kwani amefanya mzaha kwa kuwakejeli wananchi walioathirika na uchafuzi wa Mto Mara na kuzusha sintofahamu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Machi 23,2022 Msemaji wa Sekta ya Maji na Mazingira wa ACT Wazalendo, Esther Thomas amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imezembea kushughulikia tatizo hilo ambalo limeathiri wananchi, mifugo na viumbe hai vinavyotegemea maji ya Mto Mara.
Amesema ripoti zilizotolewa na Kamati mbili tofauti za uchunguzi kuhusu Uchafuzi wa Mto Mara kwa nyakati tofauti zimezua sintofahamu miongoni mwa watumiaji na wadau wengine kwa ujumla.
"Kwa mfano, ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya uchunguzi wa uchafuzi wa mazingira ya Profesa Samweli Manyele iliyotolewa Machi 19,2022 inapishana sana na taarifa ya awali ya uchunguzi wa kimaabara jambo ambalo limezua mkanganyiko miongoni mwa wadau kujua uhalisia na ukweli kuhusu taarifa hizi mbili.
"Mnamo tarehe 12 Machi, 2022 Bodi ya Maji Bonde ya Ziwa Victoria (LVBWB) ilieleza kuwa uchunguzi wa awali wa kimaabara umebaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya Mto Mara na kusababisha samaki na viumbe hai majini kufa.
" Hata hivyo katika hali ya kushangaza, ripoti ya Profesa Manyele imeonyesha sababu ni kuwepo kwa kinyesi cha ng"ombe zaidi ya tani 1.8 milioni na mkojo lita bilioni 1.5." amesema Msemaji huyo wa kisekta wa Maji na Mazingira wa ACT Wazalendo.
Mbali na hayo, ACT Wazalendo kimetaka kuwapo kwa uchunguzi wa chombo huru ambacho hakifungamani na Hii inaleta mkanganyiko miongoni mwa wadau, wananchi na wataalamu kujua uhalisia na ukweli wa taarifa hizi mbili.
"Mnamo tarehe 12 Machi 2022, Bodi ya uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya mto Mara jambo lilisababisha samaki na viumbe wa majini kufa, huku ripoti ya Profesa Manyele ikionyesha sababu ni kuwepo kwa kinyesi cha ng’ombe zaidi ya tani 1.8 milioni na mkojo lita bilioni 1.5 jambo ambalo limeongeza sintofahamu kwa jamii"amesema Esther.
Ameongeza kuwa kwa muda wote wa uchunguzi hadi sasa hakuna jitihada madhubuti zilizochukuliwa na Serikali
kushughulikia wananchi walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira wa mto Mara kwani wapo walioathirika kwa kupoteza mifugo yao kufa kutokana na kunywesha maji mifugo yao katika mto huo, wavuvi waliopoteza kipato kwa kuzuiwa shughuli za uvuvi kupisha uchunguzi. 23,2022.
No comments:
Post a Comment