HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 31, 2022

DCCP, Wejisa waungana kusafisha feri jiini Dar

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Tabu Shaibu alifagia eneo la feri.

Mwenyekiti wa DCPC, Bi. Irene Mark akizungumzia zoezi hilo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Tabu Shaibu (mwenye shati la kijani) muda mfupi baada ya kumaliza usafi eneo la feri.
Meneja wa Wejisa, Kunambi Ally akizungumzia zoezi hilo mbele ya wanahabari.


 

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC), kwa kushirikiana na Kampuni ya Wejisa wamefanya usafi kwenye soko la kimataifa la samaki wakimpongeza Rais Samia Saluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani.

Akiongoza shughuli za usafi sokoni hapo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Tabu Shaibu alisema ni jambo jema kushiriki shughuli za kijamii na kushirikiana na serikali kwa vitendo.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa usafi huo, Shaibu aliipongeza DCPC kwa kutekeleza maagizo ya serikali ya Jiji la Dar es Salaam kwa vitendo huku akiwatia shime viongozi wa klabu hiyo kuendeleza jambo hilo jema.

“Nawapongeza mmeanza vema endeleeni hivi, hatutasita kuendelea kushirikiana nanyi, huu usafi wa wote kila wiki ya mwisho wa mwezi ni agizo la mkuu wetu wa mkoa bwana Amos Makala.

“Nanyi ni mashahidi tangu tumeanza mpaka sasa tumeshuhudia kwa mara ya kwanza Dar es Salaam inaingia kwenye orodha ya majiji masafi Afrika tumeshika nafasi ya sita.

“Naamini ninyi wanahabari mkiendelea hivi ipo siku tutashika nafasi ya kwanza kwani hao walioshika nafasi ya kwanza wana nini na sisi tuna nini? Tunaweza tukiendelea kushirikiana na wadau wengine.

“Usafi ni maendeleo tuwe wasafi kila siku ila hili la mwisho wa mwezi tutoke kwa pamoja jamii ione kwamba hili sio suala la serikali ni letu sote nimefarijika sana mmekuja kivingine hongereni sana ninyi ni wadau muhimu wa jiji letu,” alisema Bi. Shaibu.

Mwenyekiti wa DCPC Bi. Irene Mark alisema hili ni zoezi litakaloingia kwenye kalenda ya shughuli za klabu hiyo hivyo kuwataka wanahabari wote wa jiji hilo kushiririkiana.

“Tunaishukuru kampuni ya Wejisa kwa kutupokea na ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji kwa kutupokea na kuahidi kushirikiana nasi huu ni mwanzo tutaendelea nakuahidi.

“Nawahimiza wana DCPC wenzangu wajitokeze kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tufanye usafi tushirikiane na serikali yetu maana usafi ni maendeleo tukishiriki kwenye maendeleo tutakuwa na habari nzuri za kuandika kwa taifa letu,” alisema Bi. Mark huku akisisitiza kumuunga mkono Rais Samia.

Meneja wa Wejisa, Kunambi Ally aliipongeza DCPC kwa kulipa kipaumbele suala la usafi hivyo kuahidi kuendelea kushirikiana nao.

Alisema eneo la feri ni muhimu kufanyiwa usafi kwa kuwa lina mkusanyiko mkubwa wa watu wa kada, rika na kariba tofauti hivyo lisipozingatiwa kwa usafi litaathiri afya za watumiaji wa eneo hilo na kwenda kinyume cha maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makalla.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni, Bi. Mwanaheri Katumbo ameipongeza DCPC kwa kushiriki usafi kwenye kata hiyo.

Aliwataka waendelee kushiriki kwenye zoezi hilo kila wakati huku akisisitiza kuwa usafi ni maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages