Na Jasmine Shamwepu
WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanatenda haki bila kujalli Mkubwa au mdogo huku akisisitiza kuwa wizara haiwezi kustawi bila ya kuwepo kwa upendo, haki na kuheshimiana.
Ameyasema hayo leo jijini hapa wakati akifungua kikao Cha Baraza la wafanyakazi kikao kilicholenga kujadili mwenendo wa utekekezaji wa bajeti ya wizara kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 na Mpango wa bajeti ya wizara wa Mwaka wa fedha 2022/ 2023 na zoezi linaloendelea la Mfumo wa Anwani za makazi.
Nnauye amesema, kwa kuzingatia uhusiano baina ya haki na Wajibu katika kutekeleza majukumu waliojipangia ni Wajibu kufahamu na kusimamia kwa ufanisi utekekezaji wa sera Mpango mkakati sheria Kanuni na miongozo taratibu mbalimbali zinayohusu haki Wajibu na stahili za wafanyakazi pamoja na Utawala bora.
"Mimi ni muumini wa haki hivyo niwaombe watumishi wote katika ngazi mbalimbali mjitahidi katika kutenda haki na Kama ukiona kwenye moyo wako haki inakusumbua kuitekeleza basi wizara hii haikufahi japa tunataka tusimaie haki," amesema
Ameeleza kuwa, kwa kuzingatia mambo hayo itawezesha kuwa na usimamizi bora wa haki na Wajibu kwa wafanyakazi na kwa ajili hivyo Baraza litakuwa kiungo mathubuti Kati ya wafanyakazi na Menejiment .
"Ni vizuri Sana kukumbuka nyinyi ni kiungo na kiungo hiki kikitumika ipasavyo wafanyakazi, kwa ajili pamoja na Baraza la kusimamia haki za wafanyakazi manufaa yataonekana hivyo mnapaswa Kama watumishi kutimiza Wajibu wenu ili kuweza kufanikisha haki hizo kupatikana kwani hakuna haki bila Wajibu,"
Na kuongeza " Baraza hili litafanya kazi bega Kwa bega Ili kuhakikisha dhamana ya Wizara iliyokabidhiwa na Serikali ya Jamhuri ya kusimia na kuongeza Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inafikiwa kwa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa letu hususani katika kuharakisha uchumi wa kidigitali.
Aidha amesema Pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakaazi kujadili na Kupitisha bajeti ya wizara ya Mwaka wa fedha,2022/ 2023 pia wizara inajivunia mafanikio walioyapata katika Mwaka Wa fedha wa 2021/2023.
Amesema wizara hiyo kwa kipindi cha muda mfupi Sana imefanikiwa kuonekana katika ramani ya wizara zinazotazwa Sana na kuonwa na Watu wengi.
Kuna mambo mawili makubwa tumefanikisha ambayo bila hayo Sekta nyingine zitasimama mambo ni ujenzi wa mkongo wa Taifa na ya pili kujenga Mfumo wa anwani za makazi.
" Kwa mujibu wa Ilani ya chama cha mapinduzi CCM tulitakiwa kujenga anwani za makazi mfumo wa kwa muda wa miaka 5 lakini imekuwa tofauti na tunajenga Mfumo kwa muda wa miezi 5 watu wamekuwa wakijiuliza maswali hivyo tukumbuke kuwa Jambo hilo halitawezekana Kama hatutakuwa wamoja tumefika mahali pazuri tathimini inaonyesha tumefikia sehemu nzuri asilimia 30 npaka 40 na tarehe 22 mwezi wa tano mwaka huu nakabidhi bila kushindwa," amesema.
Nakuongezà "Tunapokuwa tunakabidhi Mfumo huu lazima tutambuane lazima mchango wa kila mmoja uonekane katika kuhakikisha Mfumo huu unafanikiwa Jambo hilo sio dogo litabaki kwenye historia ya Vizazi ,"amesema Nnauye
Akizungumzia Siku 360 za Rais Samia Suluhu Hassan amesema wameweza kuanzishwa Mradi Mkubwa wa Tanzania ya kidigitali na Sisi Kama wafanyakazi tuliopewa dhamana kubwa tutajakikisha Tanzania ya kidigitali inawezekana.
Katika kipindi hiki Cha Mwaka mmoja na Kipindi kifupi Cha wizara hii tunajivunia mafanikio makubwa miradi inayotekelezwa nakusimimiwa na wafanyakazi wa wizara ya Habari.
Wito kwa Menejimenti kuhakikisha wizara iwe na mazingira mazuri ya utendaji kazi pamoja na mafanikio haya lazima tuendelee kupigania mazingira mazuri ya wafanyakazi mahusiano mazuri baina ya utendaji kazi wafanyakazi na kuhakikisha Haki na stahili za wafanyakazi zinatolewa kwa wakati
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi amesema kikao hicho ni kikaoo Cha Siku mbili na watapitia mwenendo wa bajeti ya Mwaka wa fedha 2021/2022 na pia Mwaka wa fedha 2022/23.
Pia maesema kujadiliana suala la anuani za makazi amesema hilo ni jukumu kubwa kwa kufanya jambo hilo kikamilifu.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa tughe tawi la habari na mawasiliano na teknolojia ya habari Laurencia Masigo amesema kwa Upande wa Tughe hatuna malalamiko Wala hoja iliyowasilishwa hiyo ni ishalla nzuri inayoonyesha utulivu na amani utawala,nakuomba wafanyakazi wote wa wizara kushirikiana Ili kuleta tija kazini
No comments:
Post a Comment