HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 25, 2022

MTAKA AWATAKA WAFUGAJI KUPIMIWA MAENEO ILI WAWEZE KUPATIWA HATI YA UMILIKI YA MASHAMBA YAO


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (pichani) amewataka wafugaji kuhakikisha kila mmoja anapima ardhi aliyokuwa nayo ili aweze kupatiwa hati ya umiliki wa mashamba ili kuepuka migogoro inayojitokeza kila mara.

Pia amewataka wafugaji kutoka kwenye ufugaji usiokuwa na tija na badala yake kufuga kisasa jambo litakalowasaidia kujikwamua kiuchumi wao na familia zao kupitia mifugo yao.

Mtaka ameyasema hayo jijini hapa,wakati akifungua mkutano baina ya wafugaji wa mkoa wa Dodoma na viongozi wa mkoa,wenye lengo la kuwaelekeza juu ya umuhimu wa ushiriki wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyiwa Mwaka huu kwa wafugaji,pamoja na utambuzi wa
mifugo.

Mtaka amesema ofisi yake itashirikiana na watu wa Idara ya ardhi kutoa kipaumbele kwa wafugaji katika zoezi zima la upimaji maeneo walionayo,kwa sababu anaamini hakuna mfugaji ambaye hamiliki ardhi.

" Hakuna kitu ambacho kinaweza kuwaokoa wafugaji kama ukiwa na hati ya kumiliki eneo ulilokuwa nalo,hivyo ni
vema mkafanya utaratibu wa kuungana kwa pamoja ili watu wa idara ya ardhi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa na idara ya ardhi waweze kuendesha kampeni ya upimaji ardhi kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma," amesema Mtaka.

Aidha alimuelekeza Mwenyekiti wa wafugaji nchini,kuwaeleze wafugaji wake juu ya umuhimu wa kuwa na ardhi ambayo imepimwa,lasivyo wataendelea kusumbuka kila iitwapo leo kwa sababu ya kukwepa sheria ya umiliki ardhi.

Amesema,hivi sasa dunia inakwenda katika ufugaji wa kisasa wenye tija,hivyo ni vema nao wakabadilika ili kuendana na wakati wa sasa,wapime mashamba yao ambayo yatawasaidia kutenga sehemu ya malisho ya mifugo.

"Ni wafugaji wachache sana ambao wanang'ombe lakini hawana ardhi,hivyo hilo ni jambo la msingi, kuchukua hatua ya kupima ardhi mliokuwa nayo ili muwe salama,"amesema Mtaka.

Amesema anahitaji kuona mfugaji anakuwa na bima ya afya,anasomesha watoto katika mazingira mazuri,anaishi sehemu nzuri kupitia ufugaji anaofanya na hiyo itakuja kama mtakubali kubadilika kufuga kisasa,japo wapo baadhi yenu wapo katika hatua hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na suala la Hereni amesema wafugaji wanapaswa kuondokana na dhana ya kupiga chapa ng'ombe kwa kutumia moto, badala yake wawavishe hereni ambazo zitawasaidia kufanya utambuzi wa mifugo waliokuwa nayo.

Mtaka amesema Ng'ombe akiwekewa hereni hata akipotea ni rahisi kumpata kwa sababu tayari anakuwa kaingia katika mfumo wa utambuzi wa mifugo.

Alifafanua zaidi ya kuwa, karne ya sasa kila kitu kwa mnyama kina thamani,ukianzia ngozi ya ng'ombe paka kwato zake.

"Na ndiomaana nimekuwa nikisisitiza wafugaji wasiweke alama kwenye ng'ombe kwa kuchoma ngozi ambayo ukitaka kuiuza utashindwa kutokana na alama aliokuwa nayo.

Kwa upande wake  Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma,Dk Fatma Mganga amewataka wafugaji kutumia elimu walioipata kuhusu ufugaji wa kisasa,ili kwenda kufanya mabadiliko ya ufugaji wanaofanya badala yake wafuge kwa tija.

Alisema wao kama viongozi,wanatamani kuona wafugaji wa Dodoma wanafuga kisasa na kuwa mkoa wenye mfano katika suala la ufugaji.

Naye mfugaji kutoka Kongwa,Yared Yacob aliushkuru uongozi
wa mkoa kutokana na kuwapa elimu ya namna ya ufugaji wa kisasa, pamoja na kuwasisitiza kuvisha hereni mifugo ili kuwatambua kirahisi.

No comments:

Post a Comment

Pages