HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 28, 2022

NMB yazindua Huduma ya Wakala kwa Simu za Mkononi

Benki ya NMB imezindua huduma maalumu ya kuweka na kutoa pesa kirahisi kupitia wakala watakaotumia simu zao za mkononi tu.

Huduma hiyo ya NMB Pesa Wakala imezinduliwa jijini Dar es Salaam, ikilenga kusogeza ‘Karibu Zaidi’ huduma za kifedha kwa wananchi, pamoja na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania, lengo likiwa kuongeza idadi ya mawakala kutoka 11,000 wa sasa, hadi 100,000 miaka mitano ijayo.

Huu ni muendelezo wa utoaji wa suluhishi za kidijitali zilizo rahisi na salama kwa wateja ili kuwafanya kuendelea kufurahia huduma zao popote walipo.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alivitaja vigezo vya mtu kuomba uwakala wa NMB Pesa Wakala kuwa ni pamoja na Leseni ya Biashara, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na simu ya mkononi ya aina yoyote (smartphone au kitochi).

Sasa Wakala anaweza kutumia huduma hii kupitia simu yake ya mkononi tu, bila kuhangaika kupata mashine za PoS ambazo zinatumia kadi. Kwa mteja, hakikisha umejiunga na NMB Mkononi kuweza kufurahia huduma hii kiurahisi.

 Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), kulia kwake Kaimu Mkuu wa Uthibiti hatari na utekelezaji, Oscar Nyirenda, Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidigitali, Kwame Makundi na Mkuu wa Idara ya Bidhaa, Aloyce Maro (kulia) Meneja Mwandamizi chaneli za huduma, James Manyama (kushoto) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya NMB Pesa Wakala.

No comments:

Post a Comment

Pages