Mbunge mstaafu wa jimbo la Kibaha vijijini wa kushoto akiwa anamkabidhi simu janja Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani wakati wa halfa fupi ambayo ilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM halmashauri na mji Kibaha.
Na Victor Masangu, Kibaha
Katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha mapinduzi (CCM) Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kushirikiana bega kwa began a Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wameamua kutoa simu janja 14 kwa ajili ya kuweza kusaidia kusajili wananchama kwa mfumo wa njia ya kielekroniki.
Koka akizungumza katika halfa hiyo ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama kutoka ngazi za Kata pamoja na matawi alisema kwamba alisema ameamua kujitolea simu hizo ili ziweze kurahisisha zaisi zoezi la kuwasajili wanachama wa zamani pamoja na wapya kwa njia ya kisasa zaidi.
“Nimeamua kukabidhi simu hizi kwa sababu jambo hili lilikuwa linatutatiza kwa mipindi cha muda mrefu kwa hiyo kata zote 14 nimezipatia simu janja hizo ambazo sasa zitatumika kuwasajili wanachama wetu wa CCM kwa njia ya kidigitali zaidi na hili jambo ni kwa ajili ya manufaa ya chama cetu cha mapinduzi,”alisema Koka.
Mbuge huyo aliongeza kuwa wakati chama kinaelekea katika kuchagua viongozi wake mbali mbali ni lazima itambue wanachama wake wamefanyiwa usajili kwa mfumo wa kidigitali ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.
Katika hatua nyingine aliwataka wanachama wote wa CCM Katika jimbo lake kuhakikisha wanazingatia kanua na sheria zilizopo ikiwa sambamba na kuwajushusha kuendelea kulipa ada na kuwataka viongozi ambao wamekabidhiwa simu hizo kuhakikisha wanazitunza vizuri na kuzitumia kwa matumizi ambayo yamepangwa na sio kuziweka kabatini.
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma alisema anatambua mchango mkubwa ambao unafanywa na chama chake hivyo akaamua kusapoti kwa kutoa simu nne kwa wanachama hao lengo ikiwa ni kupata fursa ya kujisajili kwa urahisi kwa njia ya kieletroniki.
Pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa hatua hiyo ya kutoa simu sambamba na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote wa Tanzania.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Pwani Said Goa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo alisema kwamba simu hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kufanya usajili kwa wanachama katika kata zote 14 ambazo zipo katika Jimbo la Kibaha mjini.
Goa alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ya mwisho kwenye usajili wa wanachama kwa njia hiyo kati ya Wilaya tisa za mkoa huo.
Alisema kuwa moja ya changamoto walizokuwa nazo ni ukosefu wa simu za kusajilia wanachama.
Naye Diwani wa Viti Maalum Selina Wilson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha alisema kuwa msaada huo utasaidia kwani walikuwa na wakati mgumu kujichangisha hadi kununua simu hizo.
Wilson alisema kuwa watashirikiana na viongozi wa kata ili kusajili wanachama kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM kata ya Kongowe Simon Mbelwa alisema aliwapongeza kwa dhati wabunge hao kwa kuweza kutoa simu janj ahizo ambzo zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwasajili wanachama hao.
Aliongeza kwamba malengo yao makubwa ni kuhakikisha kwamba wanawasajili wanachama wote wa CCM kwa kutumia mfumo huo wa kieletroniki na kwamba watajitahidi kupitia katika maeneo yote kuanzia kazi za mitaa.
No comments:
Post a Comment