|
Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. |
|
Mmoja wa wakilishi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akikabidhi sehemu ya msaada kwa Afisa Elimu Maalum Jiji Dar es Salaam, Bw. Swalehe Msechu (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. |
|
Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. |
|
Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (aliyesimama) akizungumza kuwakaribisha baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la TTCL walipowasilisha msaada wao kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. Kulia ni Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani na viongozi waalikwa wakifuatilia. | | | |
Na Mwandhishi Wetu
WAFANYAKAZI Wanawake toka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wametoa msaada kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam wenye mahitaji maalum ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kulisahidiakundi hilo lenye uhitaji.
Msaada huo wa vyakula kama unga wa mahindi, mchele, mafuta ya kula, sukari, chumvi, sabuni pamoja na taulo za kike kwa watoto wahitaji umekabidhiwa jana shuleni hapo na baadhi ya wafanyakazi wanawake kutoka TTCL.
Akizungumza Kiongozi wa Wanawake wa TTCL, Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu TTCL, Bi. Mercy Amani alisema akinamama hao wameguswa na changamoto wanazozipata wanafunzi wenye mahitaji maalum hivyo kuamua kujitolea kwa kuchangishana wao wenyewe na baadaye juhudi zao kuungwa mkono na menejimenti ya TTCL.
Aidha alisema TTCL inaungana na kuwashukuru wazazi, walezi, ndugu, jamaa pamoja na Serikali kwa ujumla kwa kile kuwawezesha kundi hilo maalum la watoto kupata elimu yao shuleni hapo. Aliongeza kuwa watoto hao wanaweza kufanya makubwa endapo watapata elimu yao vizuri.
Aidha, TTCL inashukuru sana kwa fursa hii mliyotupa sisi Wafanyakazi Wanawake wachache kwa niaba ya wenzetu walioko nchi nzima, kuja kuwaona watoto na kuwapatia zawadi na msaada wetu ndogo pamoja na kuwafadhili.
|
Picha ya pamoja kati ya baadhi ya Wafanyakazi Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na sehemu ya viongozi na Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam walioshiriki hafla ya makabidhiano ya msaada kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana uliotolewa na TTCL ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. |
Pamoja na hayo, Bi. Amani aliwashukuru uongozi wa shule kwa juhudi mbalimbali wanazoziweka katika kuhakikisha watoto hawa hao wanajifunza masomo darasani na kushiriki shughuli anuai za kijamii ikiwemo michezo, hali ambayo huwajenga kiafya pia.
"Taarifa zimetuonesha kuwa hii ni shule nzuri, yenye juhudi kubwa ya kuwalea vijana na kufanikisha ndoto zao za kitaaluma na ki maisha kwa ujumla. Hapa ni mahali pazuri ambapo raia wema na nguvu kazi ya nchi hii kwa siku zijazo zinaandaliwa. Hii ndio sababu ya sisi pia kuguswa na kuomba kuja kuwatembelea," alisema Bi. Amani.
Hata hivyo, aliwataka wanafunzi hao kutumia kikamilifu nafasi ya kupata elimu walioipata iwe chachu ya kufanya vizuri zaidi, na kamwe changamoto za kimaumbile na miundombinu zisiwafanye kukata tamaa bali iwe ari ya kusoma kwa bidii na kuzingatia yale yanayofundishwa na walimu na walezi na hatimaye kuzifikia ndoto zao.
TTCL ina majukumu na malengo ya kutoa huduma bora ya Mawasilino ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia inayo kampuni tanzu ya T- PESA ambayo inatoa huduma ya fedha mtandao, ambayo inawawezesha Wananchi kupata huduma mbalimbali kama Kutuma Fedha, Kulipia Ankara za huduma kama vile Maji, Umeme (LUKU), Ving’amuzi (Visimbuzi) na Kununua vifurushi vya TTCL huku huduma nyingine zikiendelea kuongezwa.
Naomba nitoe rai yangu kwenu, tuoneshe uzalendo wetu kwa kutumia bidhaa za TTCL ambazo kwa hakika ni mali halisi ya Watanzania kwa 100%. Tumia chako. Jenga kwako. RUDI NYUMBANI.
|
Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum. |
No comments:
Post a Comment