Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Tom Tao akizungumza na wadau wa kampuni mbalimbali alipokutana nao jijini Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya Huawei Tanzania imesema katika kipindi chake cha zaidi ya miaka 13
ya uendeshaji shughuli zake nchini Tanzania imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutoa mchango mkubwa kwenye huduma ya miundombinu ya Teknolojia
ya Mawasiliano (ICT) huku ikibainisha kuhudumia asilimia 75 ya
Watanzania.
Aidha, kampuni hiyo katika kipindi
hicho inajivunia kutengeneza ajira zaidi ya 1,000 zikiwemo za Wahandisi
wa Teknolojia ya Mawasiliano pamoja na utoaji mafunzo kwa vitendo kwa
wahandisi zaidi ya 2000 wa ICT.
Hayo
yamesemwa jijini humo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Nchini, Tom Tao
wakati kampuni hiyo ilipokutana na wadau wa kampuni mbalimbali lengo
likiwa kueleza bidhaa zao na kubadilishana mawazo.
Amesema
kuwa kampuni hiyo inasaidia kutatua changamoto mbalimbali za ICT
hasahasa katika Miradi ya Kimkakati ikiwemo Mradi wa Reli ya KIsasa
(SGR) hivyo inashiriki bega kwa bega na Serikali kuhakikisha mradi
unakamilika kwa haraka.
Kwa upande wake, Meneja
wa ICT wa Kampuni ya Redington- Tanzania, Rahul Bhati amesema ICT
imesaidia kukuza uchumi ikiwemo kupunguza tatizo la ajira kwani
Watanzania wanaitumia teknolojia hiyo kupashana habari na kutangaza
biashara zao.
Nae, Mkurugenzi Msaidizi wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano
na Teknolojia ya Habari, Peter Mwalyasanda ameupongeza uongozi wa
Huawei nchini kwa jitihada wanazozifanya za kukuza uchumi kupitia ICT.
Ameongeza
kuwa Serikali imefanya marekebisho katika sheria, kanuni, sera na
miongozo kwa upande wa teknolojia lengo likiwa kukuza ICT.
No comments:
Post a Comment