Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 23 kwa
tuhuma matukio ya uhalifu wa wizi na unyang'anyi wa kutumia silaha
ikiwemo visu na mapanga.
Akizungumza na
wanahabari jijini humo Kamanda wa kanda hiyo Jumanne Muliro amesema watu
hao wamekamatwa katika mwendelezo wa oparesheni kali ya mtaa kwa mtaa
pamoja na kata kwa kata inayolenga kudhibiti matukio ya uhalifu.
"
Wahalifu wanadaiwa kupanga njama za kufanya uhalifu kufikia jana Mei 12
tumewakamata wengine 23 wanaotumia silaha kufanya wizi wa kutumia
silaha," amesema Kamanda Muliro.
Amebainisha
kuwa watuhumiwa 11 waliofanya tukio uhalifu eneo la Kitunda Machi 27
mwaka huu walikamatwa na kwamba walifanikiwa kupora runinga 3 huku
akisisitiza kupitia intelejensia walitiwa nguvuni.
Kamanda
Muliro ameonya watu kuacha tabia ya kuzusha matukio ya uhalifu
wanapoona vikundi vya vijana wakiwa wanne wamekaa kwa kutoa taarifa
ambazo si za ukweli kwani zinazua taharuki na hofu kwa wananchi.
Amefafanua
kuwa vikosi vya jeshi la polisi vinaendelea kupambana na uhalifu jijini
huku akiwaonya wazazi wanaofaidika na matunda ya wizi ya watoto wao
watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment