HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 28, 2022

Kaya 300 zabainika kuweka makazi ndani eneo la mapito wanyamapori Babati



Mwandishi Wetu, Babati

Kaya zaidi ya 300 zimebainima kuishi ndani ya  eneo la ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara ambalo ni shoroba ya wanyamapori.


 Afisa Maliasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Michael Gwandu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na jitihada za mkoa wa Manyara kuendeleza uhifadhi na Utalii, alisema kaya hizo zimebainika katika uhakiki wa eneo hilo hivi karibuni.


Alisema baada ya kubainika tatizo hilo hivi sasa tathmini inaendelea ili hatua zichukuliwe katika kuhakikisha eneo hilo linalindwa kwani kama mapito hayo yakizibwa kabisa wanyama wanaweza kuathirika na magonjwa ya mlipuko.


Gwandu alisema ni muhimu mapito hayo, kubaki wazi ili kuwezesha wanyama kuweza kutembelea kuzunguka ikolojia hiyo,ambayo huwezesha kupata uzao tofauti na hivyo kupunguza athari za kuzaliana familia moja .


 “ni muhimu sana kulinda ikolojia hii kwani wanyama wanaotoka Tarangire ndio wanaozunguka hifadhi ya Manyara, Ngorongoro,mapori ya akiba ya Mkungunero na maeneo mengine hivyo tunatoa wito watu kuacha kuvamia maeneo haya”alisema

Sehemu kubwa ya mapito hayo yapo   ndani ya eneo la hifadhi ya wanyama ya Jamii (WMA) ya  Burunge ,Moja ya hifadhi za jamii zenye mapato mengi.

Katibu wa Burunge WMA,Benson Mwaise alisema uvamizi wa shughuli za kibinaadamu katika hifadhi hiyo imekuwa ni changamoto kubwa.

"Tumekuwa tukiwaondoa wavamizi wa maeneo tuliyotenga Kwa uhifadhi na mapito ya wanyama lakini baadhi wanarudi"alisema

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TAWA Kanda ya Kaskazini,Peter Mbanjoko alisema uvamizi katika maeneo ya mapito ya wanyamapori umekuwa na athari katika uhifadhi na kuchochea ujangili.

Mbanjoko alisema kuweka makazi katika eneo la  mapito ya wanyama katika ikolojia ya Tarangire- Manyara  imekuwa ikichangia matukio ya ujangili.

No comments:

Post a Comment

Pages