HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 12, 2022

Mavunde ampa mkandarasi siku 14 kukarabati skimu ya umwagiliaji Katavi

Naibu Waziri wa Mifugo, Athony Mavunde akizungumza na wananchi kuhusu uamuzi wa kumpa siku 14 mkandarasi kukarabati skimu hiyo.


Na Mwandishi Wetu


NAIBU Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amempa siku 14 mkandarasi anayetakiwa kukarabati mradi wa umwagiliaji wa Kilida uliopo katika Jimbo la Kavuu Kijiji cha Kilida, Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Akitoa maelekezo hayo katika eneo la mradi huo alipotembelea kujionea uharibifu uliotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni na kuharibu baadhi ya mashamba ya wakulima katika kijiji hicho, Mavunde amesema utekelezaji wa mradi huo uanze ndani ya siku 14 kuanzia jana.

“Awali mkandarasi alikuwa anasema anashindwa kuja sababu ya mvua ila nimefika mwenyewe hadi hapa na nimejionea barabara zinapitika na hakuna kisingizo, nampa siku 14 aje aanze kazi tuwasaidie wananchi wetu.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaongeza wigo wa kilimo cha umwagiliaji nchini ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

“Maeneo ambayo Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza tuyape msisitizo ni kilimo cha umwagiliaji, na ndio maana nipo hapa kuhakikisha skimu hii inafanya kazi kwa ukamilifu ili wananchi wengi wanufaike,” amesema Mavunde.

Awali Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mbunge wa Jimbo la Kavuu, Geophrey Pinda amesema mradi huo wa umwagiliaji utakapokamilika siyo tu utatoa ajira lakini pia utasaidia pia kuzalisha mbegu.

“Tunataka hapa pawe na mradi mkubwa wa umwagiliaji utakaosaidia uzalishaji mkubwa wa mbegu. Wananchi wa huku wanaumizwa sana na bei ya mbegu ila zikizalishwa hapa maisha ya wananchi wengi hapa yatabadilika,” amesema Mbunge huyo.

Awali mkandarasi anayesimamia mradi huo alisema anashindwa kuja eneo la mradi kutokana na mvua lakini leo (jana) amefika mwenyewe kujionea barabara zinapotoka na hakuna kisingizo.

No comments:

Post a Comment

Pages