HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2022

SHAKA ATAKA WANANCHI WAPEWE NAFASI KUSHUHUDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwa amebeba kikapu cha samaki cha mchuuzi Hamad Mustafa, alipotembea soko la samaki la Kimataifa la feri jijini Dar es Salaam.
 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amewataka viongozi mbalimbali wanaofanya ziara hususan katika miradibya maendeleo kuwapa fursa wananchi kuona kinachofanywa na serikali.

Shaka ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipotembea soko Kuu la Kariakoo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, likiwemo Soko la Kariakoo alikoshuhudia hatua nzuri za ukarabatibwake.

"Ndugu zangu viongozi nadhani sasa ni muda mwafaka kubadilika katika hizi ziara, badala ya kukaa na kujifungia na kuzungumza sisi wenyewe, ni vyema tukawapa nafasi wananchi kuona Yale yanayofanywa na serikali yao chini ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema.

Shaka ameipongeza serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika ujenzi nabukarabati wa soko hilo ambapo amesema litakapokamilika manufaa yake hayatakuwa kwa Kariakoo pekee bali ni kwa Dar es Salaam na Afrika Mashariki yote.

Awali akimkaribisha Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Ila, Ludigija Ng'wilabuzu, aliwapongeza wakandarasi wa mradi huo kwa kuutekeleza kwa kasi.

Amesema mradi huo upo chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo amesema kazi inaendelea vizuri na anaamini itakamilishwa katika muda muda wa makubaliano.


No comments:

Post a Comment

Pages