Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Shirika
la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia Kampuni ya T-PESA kwa
kushiirikiana na Kampuni ya NGASMAKE wamezindua HUDUMA YA LIPA KWA
UHAKIKA yenye lengo la kumlinda muuzaji na mnunuzi kwa pamoja kwa
wateja kwa njia ya simu.
Akizungumza na
wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa T-PESA, Lulu Mkudde
amesema huduma hiyo itaenda kuwa suluhisho la wanunuzi na wauzaji wa
bidhaa kwa njia ya mtandao kwani itasaidia kuondoa utapeli na udaganyifu
kwa watumiaji.
" T-PESA kwa kushirikiana na
NGASMAKE kwa pamoja tumefanikisha kuwezesha huduma hii ya LIPA KWA
UHAKIKA ambayo ni pekee kabisa inayowahakikishia usalama wa bidhaa zao,"
amesema Lulu.
Amebainisha kuwa huduma hiyo
iataondoa kilio cha muda mrefu cha wanunuzi wa bidhaa kutopata bidhaa
zao ingawa wamefanya malipo, kwani muuzaji atatsubiri mapka mnunuzi
apate bidhaa yake ndio fedha itaingia kwenye akaunti yake.
Amesisitiza
kuwa mfumo utamsiadia mnunuzi fedha zake kuwa salama hadi atatakopata
bidhaa au huduma na kwamba anaweza kurudisha malipo yake ikiwa bidhaa
haijawasilishwa.
Ameongeza kuwa Muuzaji
tafaidika kwa uwepo wa mfumo huo kwani atakuwa na uwezo wa kiuhakika wa
malipo mara tu wanapowasilisha bidhaa au huduma hivyo anauwezo wa
kupokea taarifa ya malipo kabla hajatoa huduma.
Ametoa
rai kwa wanunuzi wa huduam au bidhaa kupitia mitandao ya kibiashara
inayopatikana nchini kutumia mfumo huo sababu unatoa usala wa fedha za
wateja huku akiwakumbusha huduma hiyo inapatikana kwa kupiga menyu
*150*71# kisha kuchagua namba 4 yenye Huduma ya Lipa Kwa Uhakika.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NGASMAKE, Emmanuel
Ngalya amesema kampuni hiyo inatoa huduma ya mfumo wa kifedha
unaomlinda muuzaji na mnuunuzi kwa pamoja na kwamba kutokana na
changamoto nyingi za kiusalama katika biashara ya kimtandao ikiwemo
utapeli na udanganyifu wamekuja na mfumo rafiki na salama wa LIPA KWA
UHAKIKA utakaosaidia kuondoa changamoto hizo na kupata bidhaa zisizo na
kiwango.
Amefafanua kuwa mfumo huo unafanya
kazi, mnunuzi baada ya kununua bidhaa na kulipia T-PESA fedha
hazitaenda moja kwa moja muuzaji zitahifadhiwa kwenye mfumo mpka pale
mnunuzi atakapopata bidhaa yake na kuthibitisha bidhaa aliyoagiza ndio
mfumo utaruhusu fedha hizo kwenda kwa muuzaji.
Mkurugenzi
mtendaji huyo amesema mfumo huo umewekwa vizuri kwa watumiaji na endapo
watapata changamoto yoyote ya aidha kukosa huduma watapiga namba maalum
ya kituo cha huduma kwa wateja 0800110137 au kurasa za mitandao ya
kijamii.
No comments:
Post a Comment