Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu
Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Coretha Komba, akitoa hotuba yake wakati wa
kufungua mafunzo ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Shivyawata Wilaya ya Ubungo, Mussa Geuza na kulia ni Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Feisal Hassan. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
Mratibu wa Mpango mkakati huo ambaye ni Mhadhili wa Chuo
Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Feisal Hassan, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mweka Hazina wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Wilaya ya Ubungo, Hemedi Ilumba, akitoa neno la shukrani.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Wilaya ya Ubungo, Simeon Mwakatobe, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake.
Na Mwandishi Wetu
CHUO Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es
Salaam wamekabidhi mpango mkakati wa kuendeleza Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania Wilaya ya Ubungo (2022-2027) huku wakitoa
mafunzo namna ya kuutekeleza.
Akifungua
Mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk.
Coretha Komba amewataka washiriki kuitumia vema fursa hiyo ili mafunzo
hayo yaweze kuwafikia wengi na kuwawezesha kupiga hatua katika nyanja
mbalimbali za kimaendeleo.
"Tumieni fursa hii vema
kwani itakuwa na msaada mkubwa wa kuwainua. Pia ongezeni umakini Ili
lengo la semina hii liweze kufikiwa kwa maendeleo chanya na niwatakie
mafunzo mema.
Hatua hiyo
imekuja mara baada ya Shivyawata'Ubungo' kuomba mafunzo ya utunzaji wa
mahesabu, kuandika miradi na mafunzo ya uongozi kutoka kwa Chuo Kikuu
cha Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Akizungumza
juu ya mkakati huo mratibu wa mkakati huo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Feisal Hassan amesema walianza
kutekeleza mkakati huo baada ya kupokea agizo kutoka kwa uongozi wa
Chuo.
Amebainisha kuwa wanafunzi ambao wanafanya
shahada ya pili ya utawala na menegimenti walikabidhiwa jukumu na
wakajitolea kufanya kazi ya kuwasaidia Shivyawata'Ubungo kuandaa mpango
mkakati na hilo likawa sehemu ya tathimini ya masomo yao kuweza
kuwasaidia kama wanafaulu ama wanafeli.
"Bahati
nzuri wakaandaa mpango mkakati mzuri kwa ajili ya kuhusisha kuandaa
miongozo ya kutumia na maswali elekezi na vile vile kuwatembelea na
kuzungumza na wanaoshirikiana na Shivyawata." Amesema na kuongeza kuwa.
"Leo
shughuli inayofanyika ni kuwasilisha kwao huo mpango mkakati, na
uwasilishaji huo unafanyika na wao wapo wanatoa maoni yao ya mwisho,
baada ya hapo wanakabidhiwa mpango mkakati wao.
"Kuwasilisha
mpango mkakati huu ni mwendelezo wa kuwajengea uwezo Ili waweze
kujitambua na waweze kutambulika, hivyo kutekeleza majukumu yao vizuri
zaidi ukiwa ni mkakati wa miaka mitano (2022-2027).
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi walioshiriki kuandaa mpango mkakati huo Jerome
Kihaka, amesema matarajio yao ni kwa upande wa Shirikisho la watu wenye
ulemavu Shivyawata'Ubungo kutekeleza yaliyomo kwa mantiki ya kimkakati
basi wataweza kufikia malengo.
"Matarajio
yetu makubwa ni kwa upande wa Shivyawata kama wataweza kufatisha haya
maelekezo ambayo mpango mkakati umetoa kwa maana ya mantiki ya mkakati
basi kuna uwezekano mkubwa wa kufikia malengo yao.
"Shirikisho
lina dhima yake lakini Ili kuweza kuyafikia yale ni lazima kuwepo kwa
mpango mkakati sahihi. Tumeshamaliza kuwaandalia ramani ya kule
wanakotaka kufika.
Pia
ametoa wito kwa mamlaka za kiserikali kama jeshi la Polisi kuwa na sera
ya kuwasaidia katika changamoto zao wanazozipitia huko mitaani sambamba
na wadau wengine kuwa nao karibu.
No comments:
Post a Comment