HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 28, 2022

Kongamano la Connect To Connect kufanyika Septemba

 


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, lengo likiwa ni kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect.

 

Kongamano hilo pia linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA.
 

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amesema Kongamano la Connect To Connect (C2C) litafanyika kwa siku mbili tarehe 7 na 8 Septemba, 2022 ambapo nchi nyingi zinatarajiwa kushiriki ikiwa ni pamoja na nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.


Amesema kuwa Tanzania inaunganisha nchi saba za jirani ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuwa na fursa kubwa ya kupeleka huduma na kuchichimua uchumi kupitia TEHAMA.


Dkt. Yonazi ameeleza kuwa Kongamano litatoa pia fursa kwa nchi zitakazoshiriki kufanya majadiliano, kujifunza na kuweka mikakati ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchangia uchumi , kuongeza fursa za uwekezaji, ajira na elimu.
 

Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik amesema kuwa Kongamano hilo lilifanyika Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kuleta mafanikio makubwa. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano kwa mara nyingine ambapo itapaisha zaidi Tanzania kama kitovu cha mawasiliano.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa tehema Wizara hiyo Mulengwa Mnakwa amesema kongamano hilo sio Mara ya kwanza na kwamba litafanyika tarehe 7 na 8 Septemba mwaka huu Jijini Dar es salaam.


Aidha amesema wanategemea kuwa na washiriki 300 kutoka ndani na nje ya nchi,huku msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa akisema kuwa mkongo wa taifa ni Nguzo muhimu katika kujenga uchumi wa kidigital na serikali inategemea kujenga chuo kikubwa cha tehama ambacho kitasaidia vijana wengi kupata mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Pages