HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 28, 2022

Manara apewa Ubalozi BayPort Financial Services, awashauri wachezaji kutumia mitandao ya kijamii kupata kipato

 


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Taasisi ya Kifedha inayojishughulisha na Utoaji wa Mkopo kwa Watumisi wa Umma ya BayPort Financial Services imeingia Mkataba na Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara wakua Balozi wa taasisi hiyo ambapo katika kipindi cha mkataba wake atatumia mitandao ya kijamii kuitangaza taasisi hiyo kwa jamii.

Akizungumza wakati  wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo huo mbele ya Wanahabari jijini humo amesema kuwa taasisi hiyo kumpa ubalozi imempa heshima kubwa na kwa klabu yake ya Yanga pamoja na mpira wa miguu wa Tanzania kwani ilizieleka kwa wasanii ndiyo waliokuwa wakipata ubalozi kwenye makampuni mbalimbali.

"Masharti ya Bayport siyo mwiba Kwa watumishi wa Umma ambao wanalipwa na serikali pamoja na taasisi zake,hivyo nawasihi wachangamkie fursa hii ,kwani upatikanaji wa  mikopo yao ni rahisi sana na inalipwa kupitia simu ya kiganjani popote ulipo." Amesema Manara.

Amebainisha  kuwa kutokana na kukua kwa soka la Tanzania na kuheshimishwa ndiyo sababu taasisi ya BayPort Financial Services imempa ubalozi sababu ya ushawishi wake katika soka la nchi na jinsi anavyotumia mitandao ya kijamii.

Amesisitiza kuwa kuwa taasisi hiyo inatoa huduma zake kwa mujibu wa kanuni za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kwa kufuata sheria za fedha hivyo amewashauri watumishi wa umma kuitumia taasisi hiyo kama sehemu yao ya kupata mikopo ili kupunguza gharama za maisha.

Ameongeza kuwa atafanya kazi kwa ushirikiano katika chake chote cha mkataba wake hivyo atahakikisha watanzania hasahasa watumish hao wanatambua fursa za mikopo inayotolewa na BayPort.

Amefafanua kuwa kupitia ubalozi aliopewa na taasisi hiyo atafaidika yeye na  kwani itatoa mikopo kwa wataumishi wa umma na Sereikali kupata mapato.

Amewakumbusha wachezaji wa mpira wa miguu wenye majina makubwa kutumia mitandao ya Kijamii kwa ajili ya kujitangaza nakupata kipato kitakachowapunguzia ugumu wa maisha baada ya kustaafu kucheza mpira.

Ameushukuru uongozi wa klabu na wadhamini wakw wa GSM kwa kumpa fursa za kuingia mikataba ya ubalozi na kampuni tofauti bila kumbana

Kwa upande wake, Afisa Uendeshaji Mkuu wa Bayport ,Nderingo Materu amesema kuwa taasisi hiyo inatoa huduma za mikopo kwa watumishi wa umma pekee,ambapo mikopo hiyo inatolewa kwa njia ya mtandao.

Materu amesema kuwa mteja anayetaka mkopo anapaswa kupiga simu au kubonyeza *150*49# nakufuata  maelekezo ya namna ya kukidhi vigezo vya kupata Mkopo,hivyo amesema kwamba hakuna haja yakusafiri muda mrefu au kuandika nyaraka za kuomba Mkopo.

" Bayport imrahisishia mteja kupata Mkopo Kwa njia ya haraka Kwa njia ya mtandao,leo tuna mtambulisha Khaji Manara kiwa Balozi wetu kwasababu tafikisha taarifa zetu Kwa wafuasi wengi wanaomfuatilia kwenye mitandao yake ya Kijamii ikiwemo Instagram , Tweeter, na Facebook, amesema Materu.

Nae Mkuu wa Mauzo wa taasisi hiyo, Lugano Kasambala amesema kwa sasa wanatoa mikopo ya riba nafuu kwa watumishi wa umma na kwamba wanaweza kufikiria kutoa kwa watumishi wa sekta binafsi.

Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ( Call Centre), Mercy Mgongolwa awewashauri watumishi hao kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo kwani inatolewa kwa njia ya mtandao bila usumbufu wowote.


No comments:

Post a Comment

Pages