HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 20, 2022

ATCL kuendelea kuboresha huduma

 Na Hussein Ndubikile


Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesema litaendelea kuboresha huduma mbambali za shirika hilo ikiwemo kuongeza safari nyingi za nje ya nchi ili kuendana na ushindani wa  soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi ATCL,Mhandisi Ladislaus Matindi,wakati alipotembelea  Kampuni ya Uwakala wa Tiketi za Ndege  ya Skylink Travel and Tours iliyopo jijini humo.

Matindi amebainisha kuwa baada ya kufanya vizuri kwenye soko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo kwa sasa wanajiandaa kwenda nchi za Afrika Magharibi  mwakani baada ya ujio wa ndege tano hivyo jambo liliopo sasa kwa ATCL ni kutatua changamoto zinazoikabili.

 Amesisitiza kuwa  kwa sasa wamebaini kuna changamoto kwenye suala la tiketi ikiwemo Abiria kuchelewa kupata tiketi zinazochongiwa na kusuasua kwa baadhi ya kampuni za ukataji tiketi na kuwataka makampuni hayo kutatua changamoto hiyo kwa kuwataka wateja kuweka umakini katika ukataji tiketi.

Ameongeza kuwa wanafikirikia kuongeza miruko ya safari za ndani kutokana na uhitaji uliopo hivyo wataboresha huduma iendane na hadhi ya shirika hilo.

Amefafanua kuwa ziara ya kampuni hiyo imelenga kutembelea mawakala bora 10 wa tiketi za ATCL na kwamba wamebadilishana mawazo kuhusu changamoto zinazowakabili mawakala na shirika hilo.  

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Skylink Travel and Tours,Moustafa Khataw , amesema kampuni hiyo itaendelea kuboresha huduma zake ili ziweze kuendana na hadhi ya ATCL.

Mkurugenzi huyo amesema mawakala wao wataendelea kushirikiana vyema na ATCL lengo ni kulifanya shirika hilo liuzike kwenye soko la kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages