Wateja 4 kupelekwa Nchini Qatar kushuhudia Kombe la Dunia
Kaimu
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure
Paul (kushoto) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Tisha Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, baada ya timu ya Tisha kuichapa kwa mikwaju ya penalti timu ya TemboCard wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya
Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika
leo katika viwanja vya Skauti, Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA FRANCIS DANDE.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (wa nne kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (wa tano kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Kadi, Farid Seif (wa kwanza kushoto), Meneja wa Kanda ya Mashariki, Badru Idd (wa tatu kulia) na Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa Benki hiyo, Erica Mwaipopo (wa pili kulia), wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika leo katika viwanja vya Skaut, Upanga jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB,
Bonaventure Paul akizungumza wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya
Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika
leo katika viwanja vya Skauti, Upanga jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda akizungumza wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika leo katika viwanja vya Skaut, Upanga jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya CRDB imezindua Kampeni maalumu matumizi ya
kadi iliyopewa jina la “Tisha na TemboCard” inayolenga kuendelea
kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao za TemboCard
huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo kushuhudia
kombe la la Dunia litakalofanyika nchini Qatar.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo katika viwanja
vya skauti vilivyopo Upanga, Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa
Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boniventure Paul alisema,
zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia
TemboCard zao katika kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo inatarajiwa
kuchukua miezi 6 hadi mwishoni mwa mwezi Januari 2023.
“Lengo
letu ni kuona wateja na Watanzania wanaendeleza utamaduni wa kutumia
kadi zao kufanya malipo ya manunuzi na kuachana na utaratibu wa kutumia
pesa taslimu ambazo sio salama. Katika kipindi hiki cha kampeni tutatoa
zawadi kwa washindi zaidi ya 200 ambapo zawadi zenye jumla ya thamnani
ya shilingi Milioni 100 zitashindaniwa,” alisema Bonaventure.
Akielezea
kuhusu zawadi zitakazotolewa katika kampeni hiyo, Bonaventure alisema
wateja watapata zawadi mbalimbali ikiwamo kurudishiwa asilimia 10 ya
kiasi walichotumia mara baada ya kufanya manunuzi. “Kubwa zaidi ni
zawadi ya safari ya kwenda Nchini Qatar kushuhudia michuano ya Kombe la
Dunia kwa wateja 4 ambao watakuwa na miamala mingi zaidi katika kipindi
chote cha kampeni.” aliongezea.
Bonaventure
alitoa rai kwa wateja wa Benki hiyo na Watanzania kwa ujumla kushiriki
kikamilifu katika kampeni hiyo kwa kutumia kadi zao za TemboCard kwa
kufanya malipo huku akiwasihi kuendelea na utamaduni huo hata baada ya
kampeni kwani lengo ni kufanya matumizi ya kadi kuwa sehemu ya kawaida
ya miamala ya malipo ikiwa ni mkakati wa kujenga jamii yenye matumizi
machache ya pesa taslimu “cashless society”.
“Kwa
wale ambao hawana akaunti Benki ya CRDB niwashauri wafungue akaunti ili
waweze kuunganishwa na TemboCard na kuanza kufurahia huduma huku
wakijiwekea nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ikiwemo
fedha taslimu ambapo Benki itatoa kiasi cha shilingi milioni mbili kila
mwezi. Kama mnavyojua sasa hivi zoezi la kufungua akaunti
tumelirahisisha sana,” alibainisha.
“Kama
una simu janja unachotakiwa kufanya ni kupakua SimBanking App na
kufuata hatua za kufungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA na kisha
utaomba kupata TemboCard yako, kwa wale wa sio na simu janja wanaweza
kutembelea kwa CRDB Wakala au tawi la karibu wakiwa na kitambulisho cha
NIDA kufungua akaunti na kupata TemboCard kwa urahisi. Tunatamani kuona
watu wengi zaidi wakishiriki ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo,”
aliongezea.Awali
akielezea namna ya kushiriki katika kampeni hiyo na kuibuka mshindi,
Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Erica Mwaipopo
alisema wateja wanatakiwa kutumia kadi zao za TemboCard kulipia manunuzi
na huduma katika maduka, supermarkets, migahawa, hoteli na vituo vya
mafuta kupitia vifaa vya manunuzi (POS), pamoja na malipo ya mitandaoni
ikiwamo kulipia tiketi za ndege au malipo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.Benki
ya CRDB ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha huduma za kadi ‘TemboCard’
nchini mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa
upatikanaji wa huduma popote walipo. Mpaka sasa Benki ya CRDB
imefanikiwa kutoa zaidi ya TemboCard milioni 3 ikiungana na mifumo ya
malipo ya kimataifa ya Visa, MasterCard na Union Pay. Huduma za
Tembocard zimechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia jitihada za serikali
katika kuimarisha mfumo wa malipo nchini na kuongeza ujumuishi wa
kifedha “Financial Inclusion”.
No comments:
Post a Comment