Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sarah Msafiri akimkabidhi nahodha wa timu ya New generation kombe baada ya kuutwa ubingwa huo.
Na Victor Masangu, Kibaha
Timu
ya soka ya New generation Leo imeweza kuibuka kidedea kwa kuutwa
ubingwa wa michuano ya kombe la 'Samia Suluhu Cup' baada ya kuichapa
timu ya Palasupalasu kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba
la mwendapole Wilayani Kibaha.
Katika
mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kutokana na timu
zote mbili kuonyesha kandanda la aina yake katika kipindi chote cha
dakika 90 na kuhudhuliwa na umati wa mashabiki kutoka maeneo mbali mbali
ya Wilaya ya Kibaha na maeneo mengine ya jirani.
Mchezo
huo ambao ulikuwa unasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na wapenzi wa
mpira wa kandanda ulihudhuliwa pia na viongozi mbali mbali wa
dini,serikali,pamoja na wadau wa viongozi wa chama Cha mpira wa miguu
wilaya ya Kibaha (KIBAFA)
Mabingwa
katika mchezo huo ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za
wapinzani wao katika kipindi Cha kwanza ambapo bao lao la kwanza
lilifungwa kwa njia ya kawaida na bao la pili lilifungwa kwa njia ya
mkwaju wa penati.
Katika
kipindi c ha pili wapinzani wao waliweza kupata bao la kufutia machozi
ambalo lilipatikana kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wao kufanyiwa
madhambi katika eneo la hatari.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Sarah Msafiri ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika
kilele Cha michuano hiyo ambapo alisema lengo kubwa ya kuandaa
mashindano hayo kupitia sekta ya michezo ni kwa ajili ya kuhamasisha
zoezi la sensa ya watu na makazi.
"Tunashukuru
mashindano haya ya Samia Suluhu Cup' katika Wilaya yangu ya Kibaha
yamemalizika salama na kikubwa ilikuwa ni kuwakutanisha wanamichezo
kuwahamasisha kushiriki katika sensa na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa
,"alisema Msafiri.
Aidha
Mkuu huyo alisema kwamba katika michuano hiyo imeweza kusaidia kwa kiasi
kubwa tangu ilipoanza kufanyika na imeleta matokeo chanya katika
kuwaimisha wananchi na wanamichezo umuhimu wa kuhesabiwa katika sensa.
Msafiri
aliwapongeza wachezaji wa timu mbali mbali ambao wameweza kujitokeza
katika mashindano hayo ya Samia Suluhu Cup' na kwamba yatakuwa
yanafanyika kila mwaka lengo ikiwa pia ni kukuza vipajj.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha Injinia
Mshamu Munde amebainisha kwamba Maandalizi yote kwa ajili ya sensa
yanaendelea vizuri na kwamba hamasa na mwamko kwa wananchi no mkubwa.
Munde
aliongeza kuwa mashindano ya michezo ambayo yameandaliwa maalumu kwa
ajili ya kuhamasisha sensa ya watu na makazi yameleta matokeo chanya
katika suala zima la kuwapa fursa wanamichezo kutambua umuhimu wa
kuhesabiwa.
Kivumbi Cha
michuano hiyo Cha kombe la Samia Suluhu Hassan kimemalizika ambapo timu
za soka kuanzia mshindi wa kwanza hadi mshindi wa nne zimeoatiwa zawadi
mbali mbali ikiwemo mipira,jezi, medani pamoj vikombe.
No comments:
Post a Comment