Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa pamoja na mke wake Selina Koka nyumbani kwao mtaa wa Vigaeni Wilayani Kibaha na Kalani wa sensa na mjumbe wa shina la Mkoani 'A'.
Na Victor Masangu, Kibaha
Koka
ameshiriki kuhesabiwa zoezi hilo la sensa ya watu na makazi akiwa na
mke wake nyumbani kwao katika mtaa wa Vigaeni kata ya Tumbi Wilaya ya
Kibaha mkoa wa Pwani Sambamba akiwa na familia yake.
Mbunge
huyo baada ya kuhesabiwa alisema kwamba zoezi hilo limefanyika salama
na kubainisha kuwa taarifa zote ambazo ameulizwa ameweza kuzijibu
ipasavyo kwa kalani wa sensa ambaye alifika nyumbani kwake kwa lengo la
kufanya zoezi hilo.
"Tunashukuru
zoezi hili limefanyika vizuri na mm nimeweza kupata fursa ya kuweza
kuhesabiwa nikiwa pamoja na mke wangu na familia yangu na kikubwa naweza
kusema zoezi kimemalizika salama na tumetoa ushirikiano wa kutosha
katika zoezi hili,"alisema Koka.
Pia
Mbunge huyo alibainisha kuwa umuhimu wa zoezi hilo la kuhesabiwa
kutaweza kuisaidia serikali kupata takwimu halisi ya wananchi wake lengo
ikiwa ni kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Kadhalika
Koka alimpomgeza Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta chachu
ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo Sambamba na kuwahimiza
wananchi kujitokeza katika suala zima la kuhesabiwa.
Naye
mmoja wa makalani wa zoezi hilo la sensa Mariam Mohamed amesema kuwa
zoezi hilo limeanza tangu asubuhi japo kulikuwa na changamoto ya mvua
lakini wananchi wamekuwa na hamasa katika kuhesabiwa.
"Zoezi
la sensa ya watu na makazi tumelianz mapema ya asubuhi na tumepita
katika maeneo mbali mbali ikiwemo kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini
ambaye tumemkuta nyumbani kwaki mtaa wa Vigaeni akiwa pamoja na mke wake
na ametupa ushirikiano wa kutosha,"alisema Kalani huyo.
Katika
hatua nyingine mke wa Mbunge huyo Selina Koka ameeleza kuwa ameshiriki
kikamilifu katika kuhesabiwa na kwamba zoezi hilo limekwenda vizuri na
wamehesabiwa yeye pamoja na familia yake.
Pia
mama Koka alisema kwamba matarajio yake makubwa katika zoezi hilo la
sensa ni kuwa litaweza kusaidia katika kufahamu idadi ya wananchi ili
serikali iweze kupanga mambo yake ya kimaendeleo
Mjumbe
wa shina namba tatu kutoka mkoani 'A' Jestina Lewis alisema kwamba
wananchi wa Jimbo la Kibaha wameonekana kutoa ushirikiano wa kutosha kwa
makalani ambao wamekuwa wakipita katika maeneo mbali mbali.
Kadhalika
amemshukuru Mbunge wa Jimbo kwa kuweza kushiriki kikamilifu katika
zoezi hilo Sambamba wa kuwahimiza wananchi wake kuweza kujitokeza kwa
wingi katika zoezi hilo.
Katika
Jimbo la Kibaha mjini pamoja na maeneo mengine ya Wilayani Kibaha
wananchi wake tangu asubuhi wameonekana kuhamasika katika kushiriki
katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi.
No comments:
Post a Comment